Mtanzania Isack
Ibrahim Emmanuel ambaye ni Mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Liaoning jijini Shenyang nchini China ameendeleza
ubabe wake katika mchezo wa Kick Boxing baada ya kushinda katika pambano lake lingine
la la uzito wa kilo 60kg kwenye mashindano ya “Vita ya Mfalme” katka
mji wa Jiling,Jiji la Changchun, kwa kumtwanga kwa TKO mpinzani wake Li Haoran (李浩然).
Wiki iliyopita Mtanzania huyu hodari alimtoa kwa KO mwishoni
mwa raundi ya kwanza mpinzani wake aitwaye Hubulan (胡布兰).
Isack Ibrahim Emmanuel baada ya refa kusimamisha pambano baada ya kumchakaza kwa TKO raundi ya kwanza mpinzani wake Li Haoran (李浩然).











Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...