Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) amefanya mabadiliko ya Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) kuanzia leo tarehe 08 Mei, 2019.
Kufuatia mabadiliko hayo, Mhandisi Gonsalves Rwegasira Rutakyamirwa anakuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa DDCA.
Kabla ya nafasi hiyo, Mhandisi Gonsalves (juu kulia) alikua akifanya kazi Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA), akisimamia miradi ya maji ya pembezoni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Florence Lawrence, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, hatua hiyo imetengua uteuzi wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa DDCA Domina Msonge (kushoto).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...