
Ndugu Wanafamilia na Watanzania Waishio UK
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania nchini Uingereza - TZUK DIASPORA Ndugu Abraham SANGIWA, pamoja na Uongozi mzima wa TZUK wanawatakia waislam wote duniani mwezi mtukufu mwema wa Ramadan- 2019.
Uvumilivu na huruma ambavyo ni maadili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ni muhimu zaidi hivi sasa kuliko wakati wowote ule.”
Kwa mantiki hiyo Mwenyekiti Ndugu Sangiwa amesema, *“naomba tutumie mwezi huu wa kujitafakari kwa kukumbuka watu waliopoteza maisha wakati wakisaka usalama na hifadhi na tuonyeshe uungwaji mkono kwa mamilioni ambao wamefurushwa makwao au kupoteza maisha kwa sababu ya vita, ugaidi au mateso na wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na familia zao hasa watoto wadogo wasio na hatia .”*
Pia nawaomba Watanzania tunaoishi hapa UK na maeneo mengine ulimwenguni tuonyeshe mshikamano na upendo kati yetu na kwamba mwezi huu mtukufu wa Ramadhani unatuma ujumbe muhimu zaidi hii leo ya kwamba, “kile kinachotuunganisha kiimarike kuliko kile kinachotugawa.”
TZUK tupo pamoja kwa Upendo na Amani
Abraham SANGIWA
Mwenyekiti
Jumuiya ya Watanzania UNITED KINGDOM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...