NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amempa wiki moja mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,kushughulikia madokezo ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi unaoendelea wa hospital ya wilaya ya kisasa ambapo madokezo hayo yapo mezani huku ujenzi ukiwa umesimama.

Kufuatia agizo hilo ,amemtaka katibu tawala wa mkoa (RAS) kumfuatilia ndani ya siku saba kuwe na mabadiliko ,kinyume na hapo mkurugenzi huyo atakuwa ameshindwa kufanya kazi hiyo ambayo ,waziri wa TAMISEMI ,Selemani Jafo aliagiza hospitali hizo zikabidhiwe juni 25 mwaka huu.

Akizungumza wakati alipotembelea ujenzi unaondelea katika halmashauri za wilaya ya Kibaha,Ndikilo alimuelekeza mkurugenzi Butamo Ndalahwa abadilike ,afanye kazi kwa ushirikiano na watendaji wake na asiwe chanzo cha kukwamisha kila kitu.

“Maofisa ununuzi wameshamaliza kazi yao ,watendaji wameshapeleka muda mrefu taarifa za manunuzi ya vifaa vinavyohitaji lakini madokezo hayo yapo mezani hayajafanyiwa kazi ,”

Hata hivyo alisema ,katika kukabiliana na changamoto ya utoaji wa huduma ya afya kwa jamii serikali ya awamu ya tano inajenga hospitali za wilaya tatu za kisasa ,mkoani hapo ambazo zitagharimu kiasi cha sh. bilioni 4.5.

Ndikilo alifafanua, fedha zote zinazoelekezwa katika miradi hiyo muhimu zitumike kwa wakati na kwa matumizi lengwa bila kuziacha kubaki viporo.

Awali mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alieleza,alitoa taarifa ya ujio wa mkuu wa mkoa lakini mkurugenzi ametoa hudhuru yupo katika kikao na madiwani kinachohusu masuala ya fedha.

Mkuu huyo wa mkoa alisema ,ni sawa yupo kwenye majukumu yake ambayo ni muhimu lakini ziara hiyo imelenga kufuatilia hatua zilipofika ujenzi huo,hivyo alipaswa kukaimisha mtu ambae angeweza kutoa majibu ya changamoto zilizojitokeza .

Katika ziara hiyo pia alitembelea ujenzi wa hospital ya wilaya inayojengwa Lulanzi ,mjini Kibaha akiwa hapo Ndikilo alikemea baadhi ya madiwani kuacha kuingiza siasa kwenye shughuli za wataalamu na kusababisha kukwama kwa utekelezaji wa mradi huo unaoendelea kujengwa .

Aliwaasa, baadhi ya wanasiasa na watendaji kutokwamisha kwa namna yoyote miradi ya kitaifa na kimkoa kwa maslahi ya matumbo yao .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...