Waziri wa viwanda na Biashara, Josephat Kakunda 
Na.Vero Ignatus,Arusha.

SERIKALI inakaribisha Wawekezaji wa Sekta binafsi wanaotaka kufufua kiwanda cha matairi cha General Tyre kilichopo Jijini Arusha, kupeleka barua zao na kufanya mazungumzo kwenye Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), ili waweze kuingia ubia na serikali kwa ajili ya kufufua kiwanda hicho haraka iwezekanavyo.

Waziri wa Viwanda na Biashara Josephat Kakunda ameyasema hayo Jijini hapa alipotembelea kiwanda hicho na kukagua eneo la kiwanda hicho, amesema bwatapokea barua hizo na mapendekezo ya wawekezaji wa sekta binasfi hadi Agosti mwaka huu na wapo waliopeleka tayari, ili waanze mchakato wa kukifufua kwa ajili ya kuwezesha watu zaidi ya 5000 kupata ajira.

Waziri Kakunda dhamira ya serikali kufufua viwanda vyote ambavyo vimekufa na hadi kufikia Juni mwakani wawe wameanza utaratibu wakufufua viwanda hivyo na mtu asiyefahamu NDC ilipo aende ofisi z aMkuu wa Mkoa Arusha atapewa maelekezi sahihi.

Kakunda amesema Tanzania ilikuwa na viwanda 156 kati ya hivyo 88 vinafanya kazi,68 vinamatatizo na 20 vimefutwa katika orodha ya viwanda sababu ya wamiliki kuuza kwa mtindo wa rejareja.

“Lakini viwanda 48 vilivyobaki kati ya hivyo 16 vimerejeshwa serikali ambapo kati ya hivyo 32 vipo tayari katika mchakato wa kuvifufua kwa kushirikiana na sekta binafsi na wale wenye viwanda kama wanafahamu vimekufa na hawana mpango wowote wa kuvifufua serikali tutawanyang’anya ifikapo Juni Mosi mwaka huu,ila kama wanampango w akufifufua hawana shida nao, lengoi ifikapo Juni mwakani tuanze utaratibu wa kuvifufua,”alisema

Amesema kwa viwanda ambavyo vimegeuzwa makanisa hawana shida na makanisa ila watachukua na makanisa hayo watalazimika kuomba wamiliki wa viwanda waliowapatia maeneo hayo kuwapatia maeneo mengine ya kanisa.

Aidha ameipongeza serikali ya Mkoa wa Arusha kwa kulinda eneo la kiwanda hicho na kuhakikisha halijaharibiwa.Kakunda amesema kufufuka kwa kiwanda hicho sio itasaidia ajira Tanzania pekee bali hata Afrika Mashariki na Kati na nchi za Kusini mwa Afrika watanufaika.

Kuhusu katazo la mifuko alisema serikali imeweka mazingira bora ya kuhakikisha wananchi wanapata mifuko mbadala na siyo iliyokatawa kwa kuongeza uzalishaji kwenye viwanda 15 vilivyopo nchini.

“Kama jana nimetembelea kiwanda cha Hai Mkoani Kilimanjaro ambacho kinazalisha mifuko 680,000 kwa siku na pia kuagiza kiwanda cha Mgololo Iringa kiongeze uzalisha mara tatu wa malighafi za kutosha ili wenye viwanda waweze kutengeneza zaidi mifuko ya karatasi na mingine,”alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema serikali mkoani hapa, ipo tayari kutoa ushirikiano kwa serikali katika ufufuaji wa kiwanda hicho na hata ikibidi kukiwepo na uhitaji wa eneo la ziada kwa ajili ya kiwanda hicho watasaidia kupatikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...