Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo amewaagiza wakuu wa Mikoa minne iliyopo kwenye mradi wa
“lishe Endelevu” kuhakikisha kuwa mikataba hiyo ya utekelezaji wa afua
za lishe inawashukie wakuu wa Wilaya, nao wasainiane na wakurugenzi wa
halmashauri, nao pia waishushe kwa watendaji wa kata na watendaji hao
wasainiane na watendjai wa vijiji na mitaa ili utekelezaji wa mikataba
hiyo kuwa shirikishi bila ya kubagua eneo lolote la utawala.
Amesema kuwa pamoja na utekelezaji wa mradi huo, Waziri wa nchi Ofisi
ya Rais TAMISEMI kwa niaba ya Makamu wa Rais alisainishana mkataba wa
utekelezaji wa afua za lishe na wakuu wa Mikoa yote nchini ili
kuchochea utekelezaji wa shughuli za lishe hapa nchini, mkataba ambao
una viashiria kumi ambavyo vinampima Mkuu wa Mkoa kila baada ya miezi
sita na utadumu kwa kipini cha miaka minne kuanzia januari 2018 hadi
2021
“Kwa vile eneo hili ni eneo la mradi maalum, nitatamani sana niweze
kuona katika mbao za vijiji vyetu ambavyo miradi hii inatekelezeka,
tuwe na taarifa licha ya taarifa ya mapato na matumizi, kuwe na
taarifa ambayo inasema katika Kijiji X, Kijiji cha Milepa, Kijiji cha
Wampembe ama Kijiji kingine inaonesha watoto wenye udumavu ni wangapi
na watoto wenye upungufu wa damu ni wangapi, hili jambo ninlazima
tushikane kila mtu atomize wajibu wake kuhakikisha ajenda ya lishe
tunaisimamia kwa nguvu zote,” Alisisitiza.
Ameyasema hayo alipokuwa akizindua mradi wa Lishe Endelevu
unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID)
unaotekelezwa katika Mikoa minne ya Iringa, Dodoma, Morogoro pamoja na
Rukwa ikiwa ni mchango wa Serikali ya Marekani katika kuisaidia
Serikali ya Tanzania kufikia lengo la kupunguza tatizo la udumavu kwa
watoto chini ya umri wa miaka mitano kutoka asilimia 34 hadi asilimia
28 ifikapo mwaka 2021.
Akitoa salamu za mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo
alitaja baadhi ya mambo yanayopelekea wananchi wa Mkoa wa Rukwa,
hususan watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kuwa na hali duni
ya lishe huku akisistiza Utamaduni na mazoea ya wananchi wengi kutumia
aina fulani za vyakula hususan nafaka kwa muda mrefu bila kuchanganya
na makundi mengine ya vyakula, hivyo kukosa virutubishi muhimu.
“Wananchi wengi hasa wanaoishi Vijijini kutokuwa na Elimu ya kutosha
kuhusu masuala ya lishe bora.Baadhi ya akinamama na familia kwa
ujumla, kutozingatia taratibu za unyonyeshaji na ulishaji bora kwa
watoto wenye umri chini ya miaka miwili. Baadhi ya akina mama wenye
watoto wadogo kukosa muda wa kutosha wa kuwahudumia watoto wao kwa
lishe bora,” Alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirila la Maendeleo la Watu wa Marekani
Andrew Karas aliishukuru serikali kwa kuweka kipaumbele juhudi za
kuhakikisha inapunguza hali ya udumavu nchini kwa kutekeleza afua
mbalimbali kuanzia ngazi ya kitaifa hadi kwenye halmashauri huku
akimpongeza mgeni rasmi wa shughuli hiyo Suleima Jafo na Wizara ya
TAMISEMI kwa kutoa kipaumbele maboresho ya lishe.
“Sisi sote tunatambua mchango wa Lishe katika maendeleo jumuishia na
maendeleo endelevu, tunavyojua Tanzania inaendelea kukumbwa na viwango
vya juu vyua utapiamlo Mkoani Rukwa zaidi ya nusu ya watoto waliochini
ya miaka mitano wana udumavu ambayo ni asilimia kubwa zaidi nchini,
utapiamlo una athari mbaya kwa mtu binafsi, familia na taifa,
unaathiri maendeleo ya Kimwili na pia kiakili, lishe duni huchangia
kuwa na uwezo mdogo wa kujifunza,” Alisema.
Mradi huu unalenga kuongeza na kuboresha upatikanaji na utoaji wa
huduma bora za lishe katika vituo vya afya na jamii, uzalishaji na
ulaji wa vyakula vyenye virutubishi kwa wingi katika ngazi ya kaya,
udhibiti wa usawa wa kijinsia katika mapato na matumizi ya rasilimali
za nyumbani ili kuhakikisha upatikanaji wa vyakula mchanganyiko.
Shirika la maendeleo la Watu wa marekani limetenga zaidi ya dola za
kimarekani milioni 19 ili kutekeleza mtadi wa lishe Endelevu kwa
kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 katika Mikoa
minne na Halmashauri 22 za Tanzania Bara na kulenga kufikia zaidi ya
wanawake milioni 1.5 walio katika umri wa kuzaa, watoto milioni 1.1
walio chini ya umri wa miaka mitano na vijana walio katika rika la
baleghe 330,000 wenye umri wa miaka 15-19.
- Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo (kushoto) akimkabidhi mkataba wa utekelezaji wa mradi wa Lishe Endelevu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo katika hafla ya uzinduzi wa Mradi huo uliofanyika kitaifa mkoani Rukwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo (kushoto) akimkabidhi mkataba wa utekelezaji wa mradi wa Lishe Endelevu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ali Hapi katika hafla ya uzinduzi wa Mradi huo uliofanyika kitaifa mkoani Rukwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo (katikati Mwenye suti) katika picha ya pamoja na wakuu wa mikoa ya Songwe, Katavi, Iringa na Rukwa pamoja na makatibu Tawala wa Iringa, Morogoro pamoja na Waganga Wakuu wa mikoa ya Dodoma na Rukwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga muda mfupi baada ya uzinduzi wa kitaifa wa mradi wa Lishe Endelevu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (wa pili toka kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ali Hapi (wa pili toka kushoto) wakitia saini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa lishe Endelevu unaodhaminiwa na Shirika la maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) muda mfupi kabla ya uzinduzi rasmi huku nyuma yao kukiwa na makatibu tawala wa mikoa hiyo inayotekeleza mradi huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo (mwenye suti) akiwasalimia wananchi walifika kupata huduma katika banda la Taasisi ya Jakaya Kikwete kutoka kitengo cha Afya ya Moyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo (mwenye suti) akiwatunza wanafunzi wa shule ya Sekondari Kizwite waliokuwa wakitoa burudani ya wimbo wao wa Lishe Endelevu katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa lishe Endelevu uliofanyika kitaifa Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi (wa Kwanza kushoto)
pamoja na Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera wakikituza kikundi
cha Kwaya cha Laela kilichokuwa kikitoa burudani katika viwanja Ndua
Mjini Sumbawanga kulifanyika hafla ya uzinduzi wa kitaifa wa mradi wa
Lishe Endelevu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...