Serikali ya Marekani ilizindua mradi wa Lishe Endelevu katika eneo la Kizitwe manispaa ya Sumbawanga, mkoa wa Rukwa. Mradi huu mpya utasaidia kupunguza udumavu kwa watoto, kuongeza idadi ya watoto wanaopata milo yenye ubora, na kuboresha lishe kwa wanawake waliofikia umri wa kuzaa.
Lishe Endelevu, inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na kutekelezwa na Save the Children, inaonesha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Marekani na Tanzania katika kuboresha maisha ya Watanzania.
"Serikali ya Marekani inaungana na Serikali ya Tanzania kwa kutambua kuwa watoto wenye afya ni viongozi wa baadae wa Tanzania. Lishe bora itawapa watoto wa Tanzania uwezo wa upeo wao katika afya, elimu, na uzalishaji wa kiuchumi, "alisema Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Andy Karas, wakati wa uzinduzi.
Pamoja na kuboresha utoaji wa huduma za lishe, Lishe Endelevu itasaidia shughuli za maji na usafi ili kusaidia lishe bora. Mradi huu pia utaongeza upatikanaji wa vyakula kwa kukuza mazao mengi yenye virutubisho, teknolojia ya kisasa, na ufugaji wa mifugo wadogo bora kwa afya.
Kwa maelezo ya ziada kuhusu Lishe Endelevu, tembelea tovuti hii:
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...