Na Woinde Shizza Michuzi TV, Monduli.
SERIKALI ya Ujerumani kupitia Balozi wake nchini Tanzania Dkt Detlef
Waechter imekabidhi funguo za Hospitali ya Kanda ya Jeshi iliyopo katika
Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli wilayani humo iliyogharimu kiasi cha
shilingi Bilioni 5.6.
Akikabidhi funguo kama ishara ya ufunguzi na makabidhiano kwa Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Balozi Dkt Waechter alisema kuwa hospitali
hiyo ni moja ya mkataba kati ya Wizara ya Ulinzi nchini Ujerumani na
Wizara ya Ulinzi nchini Tanzania kupitia sekta ya afya huku akiahidi
kuendelea kufadhili katika miradi ya serikali ya Tanzania.
"Mradi huu ulianza 2017 ulitakiwa kuisha mwaka 2020 lakini tumeongeza muda
wa mradi hadi 2024 ili kuendelea kusaidia serikali ya Tanzania kupitia
Wizara ya Ulinzi"alisema Balozi huyo.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt Hussein
Mwinyi aliiomba Serikali ya Ujerumani kuendelea kutoa msaada kwakuwa
hospitali za Kanda hazihudumii wanajeshi pekee bali zinasaidia wananchi kwa
asilimia 80 huku wanajeshi asilimia 20.
"Wenzetu wa Ujerumani wametusaidia sana walitusaidia katika ujenzi wa chuo
cha wataalam wa tiba,vifaa na maabara na niwashukuru kwa kuongeza muda wa
mradi.....
"Lakini Hospitali hii ina vifaa bora na vya kisasa pengine kuliko hata
hospitali nyingine na itasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa
wakienda nje kutibiwa" alisema Waziri Mwinyi.
Naye Mkuu wa Majeshi nchini Generali Venance Mabeyo alisema kuwa
hadi kukamilika kwa ujenzi wa hospitali hiyo kumeghalimu kiasi cha shilingi
Bilioni 5.6 ambapo Bilioni 2.8 zilitumika kwa ajili ya vifaa tiba na Bilioni
2.8 kwa ajili ya miundombinu kwa ufadhili wa serikali ya Ujerumani.
"Aidha pia mbali na hii Walijenga chuo cha Tiba Dar es
salaam, Mbeya, Mwanza na hapa na zote ni za viwango vya juu" alisema Generali Mabeyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Tawi la Tiba wa Jeshi la Wananchi Tanzania Meja
Jenerali Denis Janga alibainisha matibabu yataanza mapema ambapo kutakuwa
na wataalam wa Idara zote ikiwemo Meno,Uzazi na picha(Xray)
huku akibainisha kuwa hospitali hii ina uwezo wa kulaza wagonjwa 50 kwa
siku na kuhudumia wagonjwa wa nje 300 kwa siku.
balozi wa Ujerumani nchini Tanzania pamoja na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa akikata utepe ishara ya kuonyesha hospital hii ipo tayari kutumika
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akionyeshwa moja ya chumba kwa ajili ya Upasuaji
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt Detlef Waechter akimkabidhi funguo za Hospitali ya Kanda ya Jeshi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi .
waziri wa ulinzi na jeshii la wananchi wa Tanzania pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania akiwa pamoja na maofisa mbalimbali wa jeshi hilo pamoja na ujerumani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...