StarTimes Tanzania imeendelea kutembelea shule za msingi jijini Dar es Salaam, ikiwa ni katika kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Siku ya Ijumaa walitembelea shule ya Msingi Taifa iliyoko Temeke jijini Dar es Salaam ambapo wawakilishi wa StarTimes walikutana na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la 4 na 5 katika shule hiyo.
Mbali na kuzungumza na wanafunzi wawakilishi wa StarTimes walitoa zawadi kwa ya king’amuzi cha Dish kwa uongozi wa shule na zawadi kadha wa kadha kwa wanafunzi waliojibu vizuri maswali na wale wanaofanya vizuri darasani.
“Ugeni wenu umewapatia wanafunzi chachu ya kujifunza Zaidi kwani kama tunavyojua watoto wanapenda hujifunza Zaidi kwa kutazama kuliko kusikiliza. Lakini pia imetusaidia kujua wapi kuna tatizo na sisi tunaweza kuongeza nguvu katika kuwafundisha wanafunzi wetu,” alisema Mwl. Mkuu wa Shule ya Msingi Taifa Bi. Juliana Lubuva.
“Lakini pia tuwapatie changamoto StarTimes wongeze maudhui ya teknolojia Zaidi kupitia katuni kwa sababu watoto wanaelewa Zaidi itawpa msukumo wa kupenda masomo ya sayansi na kupanua uelewa wao.” Aliongeza.
ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambayo wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao.
“Tunapotembelea shule hizi tunakuwa na vipengele vitatu ambavyo ni, maswali kwa wanafunzi wanaoongoza darasani, maswali kwa wanafunzi wote na kasha kuangalia katuni na maswali juu ya wahusika wa katuni an mafunzo yanayopatikana katika katuni.” Zamaradi Nzowa Meneja Maudhui, StarTimes Tanzania.
Kampeni hii ya kutembelea mashule jijini Dar es Salaam itaendelea hadi mwisho wa mwezi wa tano itafikia jumla ya shule 7 katika Wilaya 3 za Mkoa wa Dar es Salaam.
Chaneli ya ST Kids inapatikana katika kifurushi cha UHURU kilichoboreshwa kwa watumiaji wa dikoda ya Antenna na kuanzia kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa dikoda ya Dish.
Meneja
Maudhui wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa(kushoto) akimkabidhi
dishi na Dekoda la Startimes Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Taifa, Juliana Lubuva(kulia) wakati wa kutambulisha maudhui
ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za
Kiswahili.
Meneja
Maudhui wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa akizungumza na baadhi ya wanafunzi
wa darasa la 3 , 4, 5 na la 6 wa shule ya Msingi Taifa iliyoko Temeke wakati wa
kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo
yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Wanafunzi
wa darasa la 3 , 4, 5 na la 6 wa Shule ya Msingi Taifa iliyoo Temeke jijini Dar es Salaam wakiangalia katuni
zinazopatikana kwenye chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo
yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Baadhi ya wanafunzi waliojinyakulia zawadi wakiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wao pamoja na wafanyazi wa Startimes Tanzania
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Taifa, Juliana Lubuva akitoa shukrani kwa Startimes Tanzania kwa kuweza
kuwakumbuka wakati wa kukabidhiwa zawadi ya King'amuzi cha Startimes
wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo
yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Meneja Maudhui wa StarTimes Tanzania, Zamaradi Nzowa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa kwa maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili katika Shule ya Msingi Taifa iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...