Na Karama Kenyuko, Michuzi Tv
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride inayomkabili Mmiliki wa Blog 8020 Fashion, Shamim Mwasha (41) na Mumewe, Abdul Nsembo(45) umedai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya  Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Kelvin Mhina alidai kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine.

 Baada ya kueleza hayo Wakili utetezi, Charles Kisoka na mwenzake Hajra Mungula walidai kuwa shauri hilo halina dhamana hivyo wanauomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.

Wakili Wankyo alieleza kuwa amesikia kilichozungumzwa na upande wa utetezi, hivyo  watawahimiza wenzao wa upelelezi wafanye haraka na tarehe ijayo wataeleza upelelezi ulipofikia.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, 2019, washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana.

Washtakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, wanatuhumiwa kwa shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya.

Shamim na Mumewe wanatuhumiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei 1,2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini  Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...