Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii
Ukisikia na
ukifatilia unaweza ukaona kama jambo la kawaida tu katika kampeni hii ya Uzalendo
kwanza inayongozwa na Steve Mangele Nyerere ambaye kwa kipawa ameweza kukusanya
wasanii Zaidi ya 400 kutoka tasnia mbalimbali.
Nikiwa
mkoani Tanga Wilaya ya Pangani wakati wa uzinduzi wa AWESO CUP, nilipata
kusikia ushuhuda na matokeo ya ziara ya kundi hilo kwa mwaka jana katika Wilaya
ya Pangani.
Ambapo moja
ya jambo linalotajwa sana ni baada ya kutoa
msukumo wa kupatikana ujenzi wa barabara ya lami ya Tanga mpaka pangani.
Unaweza
kujiuliza je wasanii wanaweza kujenga barabara mpaka useme ziara yao kuwa
ilizaa matunda la hasha , lakini kutokana na umaharufu wao na wingi wa wafuasi
katika mitandao ya kijamii waliweza kupaza sauti na kumshawishi Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli ambapo aliagiza itangazwe tenda
mara moja hili barabara hiyo ijengwe.
Juma Aweso
ni Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa jimbo la pangani anathibitisha nguvu ya
kundi hili mbele ya wakazi wa Wilaya ya Pangani.
Aweso
anasema anawashukuru wakazi wa pangani kwa kumchangua yeye na kuwa mbunge wao
na yeye amepata marafiki kutoka uzalendo kwanza ambao kwa sasa wanaisemea vyema
wilaya ya pangani hatimaye kwa sasa Rais ameagiza barabara ya lami ijengwe
kuanzia Tanga mpaka pangani.
“tulijaribu
kwa nguvu zetu ikishindikana lakini kundi la uzalendo kwanza linaloongozwa na
Steve Nyerere lilifika hapa Panagani mwaka jana kisha kuamua kuondoka na ajenda
moja tu ya barabara ya Tanga pangani na hatimaye Rais wetu Msikivu Dr Magufuli
amekubali kujenga bara bara hii kwa kiwango cha lami na mkandarasi ameagizwa
aanze mara moja ifikapo mwezi wa tano”anasema Aweso.
Kwa upande
wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi
katika Tamasha hilo anakiri kupokea maelekezo kutoka ofisi ya Rais na kwa sasa
barabara hiyo kuanza kujengwa mapema.
“taratibu za
kutangaza tenda zilishaanza na tupo katika hatua za mwisho za kumpata
mkandarasi atakayejenga barabara hii hivyo niwatoe shaka wakazi wa pangani kuwa
ujenzi wa barabara hii utaanza mapema mwanzoni mwa mwezi May mwaka huu” amesema
RC.Shigella
RC. Shigella
anasema katika ujenzi wa barabara hiyo watamuelekeza mkandarsi ujenzi uanzie
pangani kwenda Tanga mjini kama mbunge wa jimbo hilo alivyoomba.
Akizingumza
kwa niaba ya wananchi wa Pangani Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdalah anamshukuru kiongozi
wa kundi la uzalendo kwanza na wasanii wote pamoja na wadau wengine waliofika
pangani na kuendelea kuitangaza vyema wilaya hiyo.
Dc.Zainab
anasema kuwa wapo wasanii lakini Steve Nyerere amekuwa na moyo wa kipekee na
mzalendo kwa nchi yake kuliko vile wwatu wanavyofikiri.
Anasema kuwa
sio jambo dogo kwa mtu kuweza kuwashawishi wasanii wenzio waweze kusafiri na
kuja kujitolea kufanya hamasa katika wilaya ya pangani na kuacha raha na
starehe zilizopo Dar es Salaam.
Anataja kuwa
nchi ya marekani imekuwa ikipata umaharufu kutokana na wasaniii wan chi hiyo
wanavyoweza kujivunia mambo yaliyopo nchini kwao hivyo Steve kupitia uzalen do
kwanza amechagua njia iliyobora ya kuzungumzia kazi zinazofanya na rais wetu na
kutoa hamasa kwa maeneo yaliyopo pembezoni kama pangani.
Akziungumza
kwa niaba ya Wasanii wenzie Steve Nyerere ametaja kuwa upendo wa Wasanii kwa
nchi yao ndio kitu pekee ambacho kinawafanya watoke kwenda sehemu kama hizo
kutoa hamasa.
Anasema
Wasanii wa kundi la uzalendo kwanza wametambua kuwa umaharufu wao umetokana na
watu hivyo ni wakati wa wao kurudi kwa jamii kusema asante na kuwa daraj akw
aajili ya kutatua matatizo yao.
“sio muda
wote waytanzania wanatakiwa kuelezwa juu ya nchi yao kwa lugha ngumu kuna muda
wanahitaji waambiwe kwa lugha nyepesi kupitia uwasilisho wa Sanaa na wanaelewa
haraka na kuendelea kumuunga mkono Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli” anasema
Nyerere.
Anataja kuwa
Rais Magufuli anamuda wa kuzunguka katika maeneo yote haya kuzungumza
yaliyyotendeka lakini sisi kama wasanii wazelendo tunaweza kufika na kuwa sauti
yake na ujumbe ukafika haraka sana.
Mwenyekiti wa Kundi la Uzalendo Kwanza Steve Nyerere akizungumz ana wakzi wa Pangani
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shegella akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Uzalendo kwanza Steve Nyerere
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...