Na Hussein Stambuli, Morogoro
Wadau
wa tasnia ya habari nchini wameombwa kutumia maarifa yao kuielimisha
zaidi jamii juu ya uwepo wa watu wanaoishi na ualbino kwani
mpaka sasa bado kumekuwa na changamoto ya unyanyapaa dhidi ya watu hao
ikiwemo
ushirikishwaji wao katika ajira, kuendelea kuwepo kwa matukio machache
yanayohusishwa na utekaji pamoja na kuitwa majina yasiyofaa katika jamii
wanazoishi jambo linaloashiria unyanyapaa dhidi yao.
Maombi hayo yamefikishwa na Afisa mlaghibishi kutoka
shirika la kimataifa lisilokuwa la kiserikali la kutetea usalama, ustawi na
haki za watu wenye ualbino la ‘Under the
same Sun’ Kondo Sefu ambapo amesema bado jamii imebaki katika mkondo usio
salama dhidi ya watu hao ikiwemo muendelezo wa matukio machache yanayohusishwa
na Imani za kishirikina pamoja na ubaguzi.
“Bado hali haijakaa sawa kumekuwa na matukio ya
kufukuliwa kwa mifupa ya watu wenye ualbino kwenye makaburi wanayozikwa, majaribio
ya kutekwa katika baadhi ya mikoa hili jambo bado linaonesha changamoto ya
kurejesha usawa dhidi ya watu wenye ualbino katika jamii bado inahitajika”
alisema Kondo
Awali akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa
shirika hilo la under the same sun Berthasia Ladislaus alisema kuwa shirika
hilo kwa kushirikina na serikali limeweza kusaidia kupunguza matukio ya mauaji
na vitendo vingine vya kikatili dhidi ya watu wenye ualbino.
“katika kipindi cha Januari hadi Mei kumekuwa na
matukio mawili tu ya matishio ya utekaji wa watu wenye albino katika maeneo ya
Ngorongoro na Kwimba ambapo watu wasiojulikana walitaka kuwadhuru watoto wawili
wenye albino hata hivyo majaribio hayo hayakufanikiwa” alisema Berthasia.
Pia shirika la kimataifa lisilokuwa la kiserikali la
kutetea usalama, ustawi na haki za watu wenye ualbino la ‘under the same sun’ limewaomba waandishi
wa habari kuwa na matumizi sahihi ya lugha wanaporipoti juu ya kundi hilo hasa
kuwaita ‘watu wenye ualbino’ badala ya zeruzeru, albino, watu wenye ulemavu wa
ngozi pamoja na kufanya Makala maalum juu ya maisha na changamoto wazozipitia jamii
ya watu hao.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la under the same sun Berthasia Ladislaus akifafanua jambo mbele ya wahariri mbalimbali waliojitokeza katika semina elekezi juu ya watu wenye ualbino
Wadau wa shirika la kimataifa lisilokuwa la kiserikali la kutetea usalama, ustawi na haki za watu wenye ualbino la ‘under the same sun’
Wadau wa tasnia ya habari wakiwa katika picha ya pamoja katika semina elekezi inayohusu namna ya kuripoti habari za watu wenye ualbino kwa wahariri




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...