Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la usajili wa alama za vidole lenye lengo la kuimarisha usalama kwa raia wa nchi ya Kenya wanaoishi ndani na nje ya nchi mapema leo jijini Dar Es Salaam. Waliosimama nyuma ni baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi huo waliokuwa wakisamamia zoezi hilo.
Mary Njoroge (kushoto) raia wa Kenya anaeishi nchini Tanzania akipewa maelekezo na Balozi msaidizi, Rose Mugo, wakati wa zoezi la usajili wa alama za vidole kwa raia wa Kenya linaloendelea katika ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo linalenga kuimarisha usalama kwa raia wa Kenya wanaoishi ndani na nje ya nchi hiyo. Aliyesimama kulia ni Balozi wa Kenya nchini, Mh Dan Kazungu.
Philip Wandela Mwakimu (kushoto) raia wa Kenya anaeishi nchini Tanzania akipewa maelekezo na Balozi msaidizi, Rose Mugo wakati wa zoezi la usajili wa alama za vidole kwa raia wa Kenya linaloendelea katika ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo linalenga kuimarisha usalama kwa raia wa Kenya wanaoishi ndani na nje ya nchi hiyo. Aliyesimama kulia ni Balozi wa Kenya nchini, Mh Dan Kazungu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...