TOTTENHAM HOTSPURS imeonesha kabumbu la kuvutia sana katika Champions league ya mwaka huu na kwa hakika kuna kila dalili ya kutwaa ndoo ya Champions Lg pale Estadio Metropolitan, Madrid Juni 1, 2019.
Katika michuano hii, SPURS ilipangwa kundi gumu lililowajumuisha Barca na ilipigwa mechi 3 za mwanzo lakini ikakomaa hadi kupenya!
SPURS iliwatandika Mabingwa wa Uingereza MAN CITY ambao wao ndoo ya Champions league miaka nenda miaka rudi wanaitazamia runingani tu!. Halikuwa jambo rahisi.
SPURS imewatoa AJAX timu iliyowavua ubingwa Real Madrid na Juventus iliyo na Mnyama CHRISTIANO RONALDO.
SPURS ikiwa na kocha wa kiwango cha juu, MAURICIO POCHETINO, imekuwa ikipiga kabumbu la uhakika na hainaga ujinga wa kupaki basi unaoboa maelfu ya watazamaji uwanjani na mamilioni runingani!
SPURS wana nafasi kubwa sana ya kunyakua ndoo hiyo ya CL hasa kwavile inakutana na JURGEN KLOPP's LIVERPOOL.
KLOPP ana gundu kubwa na fainali kwani katika fainali zake 7 akiwa Borrusia Dortmund na Liverpool, ameshinda moja tu na kuangukia pua katika fainali SITA!!.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...