Na.Vero Ignatus,Machame ,Kilimanjaro
Waziri
mkuu wa Tanzania Kasimu Majaaliwa, ameongoza maelfu ya watanzania
katika mazishi ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu ukanda wa Afrika
mashariki, Dr. Regnald Mengi, ambaye amezikwa leo katika makaburi ya
familia nyumbani kwa wazazi wake kijiji cha Kisereni Machame mkoani
Kilimanjaro Km 35 kutoka Moshi mjini.
Akitoa
salamu za rambi rambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania , Waziri Mkuu Kassim Majaaliwa amesema kuwa taifa litamkumbuka
Dkt. Mengi kwa mchango wake mkubwa wa kukuza uchumi nchini hasa katika
sekta ya madini, habari, viwanda na mazingira, kwani amewahi kuwa
mwenyekiti wa abaraza la mazingira Taifa.
Waziri
mkuu Majaaliwa amesema mchango wa Dkt.Mengi katika kuwakumbuka watu
wenye mahitaji maalumu utaendelea kukumbukwa daima kuindokewa na mtu
mzalendo katika historia ya Tanzania
"Hakuna
Mtanzania asiyejua mchango alioutoa kwa Taifa hili,kwa namna
alivyoguswa katika nyanja mbalimbali kwa jamii na hata kwa serikali,
tunatambua mchango wake"alisema Majaliwa.
Amesema
kuwa kama Taifa la Tanzania msiba huo wa Dkt Reginald Mengi alikuwa ni
mtu wa upendo na hakuwa na ubaguzi hivyo pigo na wameondokewa na mtu
aliyekuwa muhimu maishani na Mungu alimbariki na yeye akawa baraka kwa
wengine.
Akitoa
mahubiri katika ibada ya mazishi hayo iliyofanyika katika kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Tanzania KKKT Usharika wa Moshi mjini, Askofu mkuu
wa Kanisa hilo Dkt. Fredrick Shoo, amewaasa viongozi wa serikali hasa
wale wenye umri mdogo kuacha kiburi cha madaraka na badala yake watende
haki kwa wananchi wote bila upendeleo na watapata za Mungu.
Dkt
Shoo amemtaja Marehemu Mengi kuwa hakuwabagua maskini japo alikuwa na
tajiri na tabia hiyo inapaswa kuigwa na watu wote wenye nafasi za
uongozi serikalini, wenye madaraka na wenye pesa.
Askofu
Dkt. Shoo ameendelea kusisitiza kuwa kama Taifa la Tanzania linahitaji
kupokea baraka kutoka kwa Mungu ni muhimu kuacha ubaguzi, kiburi na
kujikweza,amekemea baadhi ya tabia ya kauli za viongozi ambazo zinaweza
kuleta migogoro katika jamii.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzania nchini Tanzania
Freeman Mbowe, amekemea tabia ya ubaguzi wa ukabila unaooneshwa na
baadhi ya viongozi na kwamba ili kumuenzi Mengi ni muhimu kuyaacha
matendo hayo kwani alikuwa ni mtu wa kujishusha japo alikuwa Bilione.
Katika
hatua nyingine Askofu Dkt.Shoo amewataka Watanzania kuacha tabia ya
kubaguana kwani ni dhambi mbele za Mungu ,wenye nafasi kuwakandamiza
wale walio wa hali ya chini,amewataka kuacha kiburi
"Hivi
nyie viongozi haswa vijana mnapopata cheo mnajisahau wanaojitutumua
kama chatu wakumbuke kuwa kila siku tunamuomba Mungu na lazima Mungu
atawashusaha"
Kwa
upande wake Waziri mkuu Kassimu Majaliwa ametoa pole kwa familia ya
Marehemu Dkt.Regnald Mengi kwa kuondokewa na mpendwa wao,amesema
amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya msiba wa Mengi
Tujifunze
kuwathamini watu wasio na uwezo katika jamii na Taifa kwa ujumla
msikivu ,mpenda amani,na mwenye kuwasaidia wengine 1990 alianza kupata
chakula cha pamoja na watu wenye ulemavu.
Kwa
upande wake Mkuu CCM Taifa Bashiru Ally amesema mchango wa Dkt. Mengi
katika Taifa haswa katika mazingira alisisitiza kupanda na kuotesha
mingi tumuenzi na kupanda miti ya kutosha
"Baba
Askofu hatujafanya kazi ya kuwaandaa vijana wetu kuwa Viongozi bora,
sasa tunavuna matunda yake, naomba nimuombe msamaha kijana wangu
Makonda, nilimsema Simiyu mara ya kwanza, akaja ofisini analia, ameanza
kujirekebisha" alisema Bashiru
Akitoa
salamu kwa niaba ya Bunge Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amesema
kuwa ameonyesha kwa hali na mali alikuwa na mali ila mkarimu na
amefanya mengi ya heshima kubwa,alijitoa bila kujali alipanda miti zaidi
ya milioni ishirini siyo jambo la kawaida.
"Nawaomba
wananchi wenzangu msiamini kila kitu kinachoandikwa kwenye mitandao ya
kijamii ,vingine vya uongo sana.alisema Ndugai
Kwa
zaidi ya mzee mmengu ameshatangulia mbele za haki haitajalisha
tutazungumza maneno mazuri kiasi gani ,tutakachoweza ni kuyaishi ya mema
aliyotenda,alikuwa mnyenyekevu,kauli zake zilikuwa za
kujenga,kupatanisha,mamlaka, fedha zinajenga kiburi zisipotumika vizuri,hakuwa kiongozi wa serikali
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu
Dkt Reginald Mengi wakati wa mazishi,Machame mkoani Kilimanjaro
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...