*Ni kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 ...yaweka wazi mikakati yake
*Yataja miradi mikubwa mitatu ya kimkakati ambayo lazima itekelezwe
*Yazungumzia hali ya upatikanaji umeme nchini, hatua itakazochukua
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Nishati Dk.Medrard Kalemani amesema kuwa Bajeti ya mwaka 2019/20 kwa Wizara hiyo inalenga kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha inazalisha umeme wa kutosha, wa uhakika, unaotabirika na wenye gharama nafuu na kwamba katika mwaka 2019/20, Wizara inakadiria kutumia jumla ya Sh.trilioni 2.142 ikilinganishwa na Sh.trilioni 1.692 iliyotengwa kwa mwaka 2018/19, sawa na ongezeko la asilimia 26.6.
Kwa mujibu wa Dk.Kalemani ni kwamba ongezeko hili limetokana na kuanza kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa Rufiji utakaozalisha MW 2,115. 166 huku akieleza katika bajeti hiyo pamoja na mambo mengine imelenga kuimarisha shughuli za utafutaji na biashara ya mafuta na gesi asilia pamoja na kuwezesha wananchi kunufaika na rasilimali hizo.
Akizungumza leo Bungeni wakati akiwasikilisha Bajeti ya Wizara ya Nishati, Dk.Kalemani ameliambia Bunge kuwa lengo bajeti hiyo ni kuiwezesha Serikali kufikia azma ya kujenga uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kuongeza fedha nyingi za ndani za miradi ya maendeleo zilizotengwa kwa mwaka 2019/20 zimeelekezwa katika miradi mitatu (3) ya kimkakati ambazo ni 117 Sh. trilioni 1.86, sawa na asilimia 95.1 ya bajeti yote ya ndani.
Ameitaja miradi hiyo ni Mradi wa Kuzalisha Umeme katika Mto Rufiji, wenye Mewati 2,115 (Sh. trilioni 1.44); Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (Sh.bilioni 363.11); na Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Kinyerezi I Extension Megawati 185 (Sh. bilioni 60).
"Mheshimiwa Spika naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe bajeti ya jumla ya Sh. 2,142,793,309,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na taasisi zake. Mchanganuo wa fedhahizo ni kama ifuatavyo: (i) Sh. 2,116,454,000,000 sawa na asilimia 98.8 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
"Kati ya fedha hizo za maendeleo, Sh.1,956,372,000,000 ni fedha za ndani na Sh. 160,082,000,000 ni fedha za nje; na (ii) Sh. 26,339,309,000 sawa na asilimia 1.2 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Sh. 15,025,821,000 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Sh. 11,313,488,000 kwa ajili ya mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara na 118 Taasisi zilizo chini yake. Naomba tena nitoe shukrani zangu za dhati kwako na kwa Wabunge wote kwa kunisikiliza,"amesema Dk.Kalemani wakati anawasilisha bajeti ya wizara hiyo.
Awali akifafanua zaidi kuhusu bajeti hiyo ambayo pia inapatikana katika Tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.nishati.go.tz. Dk.Kalemani amesema anaungana na Mawaziri wenzangu, Wabunge na Watanzania kwa ujumla kumpongeza Rais Dk. John Magufuli kwa maelekezo yake thabiti yanayonisaidia kuisimamia vema Sekta ya Nishati na ni dhahiri kuwa Rais wetu amekuwa chachu katika kutekeleza mipango mikubwa na yenye tija katika Sekta ya Nishati hapa nchini.
Amesema mipango hiyo ni pamoja na kuanza kutekeleza mradi mkubwa wa kielelezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (MW 2,115) na amewaahidi Watanzania kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Bunge na wadau mbalimbali watasimamia vema mradi huo ili ukamilike kwa wakati.
"Nitumie fursa hii kuwashukuru Makamu wa Rais SamiaSuluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa miongozo mbalimbali wanayonipatia katika kusimamia Sekta ya Nishati. Nikiri kuwa maelekezo na miongozo ya viongozi wetu hawa ni msingi wa mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Sekta ya Nishati. Aidha, napenda 3kumpongeza pia Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuendelea kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,"amesema.
Akifafanua zaidi kuhusu bajeti ya mwaka 2019/2020,Dk.Kalemani pamoja na kuelezea utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/2019 amesema kutokana na mafanikio makubwa ambayo yamepatikana ndani ya Wizara hiyo kwa bajeti iliyopita, ni matarajio kuwa TANESCO itaweza kuanza kutoa gawio Serikalini katika kipindi cha Mwaka 2019/20.
Kuhusu taarifa utekelezaji wa shughuli za wizara kwa mwaka 2018/2019 na mpango wa bajeti kwa mwaka 2019/20 amesema katika mwaka 2019/20, Wizara ya Nishati itaendelea kutekeleza maeneo ya vipaumbele mbalimbali yakiwemo: kuongeza uzalishaji wa umeme nchini ili kufikia lengo la kuwa na MW 10,000 ifikapo mwaka 2025, kwa kutekeleza miradi 18 mikubwa ikiwemo: mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji (MW 2,115) na mradi wa kufua umeme kwa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi I - Extension (MW 185).
Pia mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo MW 80, Ruhudji MW 358 na Rumakali MW 222; Kuimarisha mifumo ya usafirishaji wa umeme nchini kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa North - West Grid Extension kV 400 yenye umbali wa kilomita 1,384 inayojumuisha Iringa – Mbeya – Sumbawanga – Mpanda – Kigoma hadi Nyakanazi; Singida – Arusha – Namanga kV 400, kilomita 414; Rufiji - Chalinze – Dodoma kV 400, kilomita 512; Rusumo – Nyakanazi kV 220, kilomita 98; Geita – Nyakanazi kV 220, kilomita 133; Tabora – Urambo – Kaliua – Nguruka hadi Kidahwe Mkoani Kigoma kV 132, kilomita 391; na Tabora – Ipole – Inyonga hadi Nsimbo (Katavi) kV 132, kilomita 381. 17.
Dk.Kalemani amesema maeneo mengine ya kisekta yatakayozingatiwa na Wizara ni: kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya Mradi Kabambe wa Kupeleka Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), katika vijiji takriban 1,990 vilivyobaki 19 kati ya vijiji 12,268; kuendelea na utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania (East African Crude Oil Pipeline - EACOP); kuimarisha shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia; kuongeza kasi ya usambazaji wa gesi asilia; kuendeleza miradi ya nishati jadidifu (jotoardhi, upepo na jua); kuvutia uwekezaji katika sekta ya nishati; na kuendelea kuimarisha utendaji wa Taasisi za TANESCO, TGDC, REA, TPDC, PURA na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja ili kuongeza ufanisi na ushindani katika Sekta ya Nishati. 1
Ameongeza pamoja na maeneo hayo ya kisekta, Wizara itazingatia maeneo mengine ya kuboresha utendaji ambayo ni pamoja na: kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara na Taasisi zake katika kusimamia Sekta ya Nishati; kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa Wizara na Taasisi zake ili kutoa huduma bora zaidi; na kuendelea kuelimisha umma na kuboresha mawasiliano kati ya Wizara na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya nishati.
HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME NCHINI
Wakati huo huo Dk.Kaleman wakati anawasilisha bajeti hiyo amesema kwa sasa hali ya umeme nchini imeendelea kuimarika katika kipindi chote cha mwaka 2018/19. Aidha, mahitaji ya umeme nchini yameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na kukua na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi zinazohitaji nishati ya umeme wa kutosha, wa uhakika na wa gharama nafuu katika uzalishaji.
" Katika mwaka 2018/19 uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme (installed capacity) nchini umeongezeka na kufikia MW 1,601.90 kutoka MW 1,517.47 zilizofikiwa mwaka2017/18 sawa na ongezeko la asilimia 5.6. Kati ya jumla ya MW 1,601.90 zilizopo nchini, MW 1,565.72 zimeunganishwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa na MW 36.18 zipo nje ya mfumo wa Gridi ya Taifa.
"Matumizi ya juu ya umeme yamefikia MW 1,116.58 ukilinganisha na MW 1,051.27 zilizofikiwa mwaka 2017/18 sawa na ongezeko la asilimia 6.2. Aidha, umeme uliozalishwa nchini uliongezeka kutoka GWh 7,114 mwaka 2017 na kufikia GWh 7,374 sawa na ongezeko la asilimia 3.7. Hadi kufikia mwaka 2015, nchi yetu ilikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 1,204 ikilinganishwa na uwezo wa sasa wa MW 1,601.90 sawa na ongezeko la asilimia 33. Katika kutimiza azma ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda, Serikali kupitia Wizara ya Nishati imelenga kuzalisha umeme wa MW 10,000 ifikapo mwaka 2025,"amesema.
MIRADI YA KUZALISHA UMEME
Kuhusu Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Mto Rufiji (Rufiji Hydro Power Project) – MW 2,115 21, Dk.Kaleman amaesema mradi huo unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa Megawati 2,115 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji na mkataba wa ujenzi huo ulisainiwa Desemba 12 , 2018 kati ya TANESCO na Mkandarasi Kampuni ya Arab Contractors na Elsewedy Electric za nchini Misri.
"Tukio hili lilishuhudiwa na Rais Dk.Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Misri. Mkandarasi huyo alikabidhiwa eneo la mradi tarehe 14 Februari, 2019 na kuanza utekelezaji wa kazi za awali. Katika kipindi 22 cha mwaka 2018/19, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa miundombinu wezeshi ikijumuisha: njia ya kusafirisha umeme wa MW 8 yenye msongo wa kV 33 kutoka Msamvu, Morogoro hadi eneo la mradi yenye urefu wa kilomita 170; barabara za kiwango cha changarawe za Ubena – Zomozi na Kibiti – Mloka hadi eneo la mradi; mifumo ya maji; mawasiliano ya simu; na nyumba za kuishi Mkandarasi.
"Vilevile, kulingana na mahitaji ya umeme wakati wa ujenzi, TANESCO imeanza ujenzi wa njia ya pili ya umeme msongo wa kV 33 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Gongo la Mboto kupitia Kisarawe hadi eneo la mradi urefu wa kilomita 245 itakayosafirisha umeme wa MW 22.Katika kipindi cha mwaka 2019/20 Serikali itaendelea na utekelezaji wa mradi huu muhimu ambapo kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kuanza ujenzi wa bwawa (main dam and spillways); kuanza ujenzi wa njia za kupitisha maji (tunnels); na kukamilisha ujenzi wa njia ya pili ya umeme msongo wa kV 33 kutoka Gongo la Mboto. Fedha za ndani Shilingi trilioni 1.443 zimetengwa katika mwaka 2019/20 23 kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo.
"Utekelezaji wa mradi umeanza Desemba, 2018 na unatarajiwa kukamilika Juni, 2022. Kwa ujumla Serikali imedhamiria kwa dhati kutekeleza mradi huu bila kuyumbishwa, kucheleweshwa wala kukwamishwa na mtu yeyote kutoka ndani au nje ya nchi asiyeitakia mema nchi yetu. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rusumo – MW 80 23,"amesema.
Ameongeza kuwa mradi huu wa nchi tatu (3) za Tanzania, Burundi na Rwanda unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 80 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera kwa mgawanyo sawa kwa kila nchi. Kwa upande wa Tanzania, Mradi unagharimu Dola za Marekani milioni 113 sawa na takriban Shilingi bilioni 261.75 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
Amefafanua kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni pamoja na: kukamilika kwa ujenzi wa barabara za kuingia eneo la Mradi; kukamilika kwa ujenzi wa kikinga maji (coffer dam) na kukamilika kwa uchimbaji wa eneo la kusimika mitambo (power house). Wakati kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni pamoja na kujenga miundombinu ya kukinga na kuingiza maji katika handaki (Dam and Intake); ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme (powerhouse); ufungaji wa mitambo katika kituo cha kuzalisha umeme; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme (Switchyard);
Na kukamilisha miradi ya kijamii kwa wananchi wanaozunguka eneo la mradi (Local Area Development Plan – LADP na Livelihood Restoration Program - LRP). Fedha za nje Shilingi bilioni 3 zimetengwa na Serikali katika mwaka 2019/20 kwa ajili ya mradi huu. Mradi huu umeanza mwaka 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2020. Pia mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Ruhudji – MW 358 25.
"Mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa MW 358 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhudji mkoani Njombe. Ujenzi wa mradi huu utahusisha njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 170 kutoka Ruhudji hadi kituo cha kupoza umeme cha Kisada mkoani Iringa. 25 Katika mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: Serikali kuanza majadiliano ya ufadhili na Serikali ya China kwa ajili ya kutekeleza mradi; na kumpata Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kuhuisha Upembuzi Yakinifu.
"Ujenzi wa mradi unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani milioni 407.40 sawa na takriban Sh. bilioni 943.70 na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani milioni 53.2 sawa na takriban Shilingi bilioni 123. Katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kukamilisha taratibu za ufadhili wa mradi; kuhuisha Upembuzi Yakinifu (Updating of feasibility study); kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; na kumpata Mkandarasi wa kujenga mradi.
"Jumla ya Sh.bilioni 12.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Sh.bilioni 10.00 ni fedha za ndani na Sh.bilioni 2.50 ni fedha za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Mei, 2020 na kukamilika mwezi Aprili, 2023. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rumakali – MW 222 27. mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 222 kwa kutumia maji ya Mto Rumakali mkoani Njombe na njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 150 kutoka katika mitambo hadi kituo cha kupoza umeme cha Iganjo mkoani Mbeya,"amesema.
Amefafanua kuwa gharama za mradi huo kwa pamoja zinakadiriwa kuwa jumla ya Dola za Marekani milioni 344.22 sawa na takriban Shilingi bilioni 899.27. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kumtafuta Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kuhuisha Upembuzi Yakinifu wa mradi uliofanyika mwaka 1998; na kuanza usanifu wa miundombinu ya mradi. 28.
Wakati katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kuhuisha Upembuzi Yakinifu ; kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi; kufanya tathmini ya athari za mazingira na kijamii (ESIA); na kulipa fidia. Jumla ya Shilingi bilioni 3.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo.
" Kati ya 27 fedha hizo Shilingi bilioni 1.0 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.50 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Januari, 2021 na kukamilika mwezi Juni, 2023. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kakono – MW 87 29. Mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 87 kwa kutumia maji ya Mto Kagera na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 220 kutoka Kakono hadi Kyaka yenye urefu wa kilomita 38.8.
" Gharama za ujenzi wa mradi ni Dola za Marekani milioni 380 zitakazotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD). Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni pamoja na: kukamilisha utafiti wa kijiolojia na haidrolojia; kukamilisha usanifu wa awali wa mradi; kufanya maandalizi ya zabuni kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa Ujenzi; kuhuisha tathmini ya athari za mazingira na kijamii (updating ESIA); na kukamilisha mpango wa kuhamisha wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi (Resettlement Action Plan - RAP).Katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kutwaa ardhi na kulipa fidia katika eneo la mradi; na kutafuta Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi na njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 220.
"Jumla ya Sh.bilioni 2.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Sh.milioni 500 ni fedha za ndani na Sh. bilioni 2 ni fedha za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza Desemba, 2019 na kukamilika Desemba, 2022. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Malagarasi – MW 45 31. Mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 45 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Malagarasi mkoani Kigoma na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 132 yenye urefu wa kilomita 53 kutoka Malagarasi hadi Kidahwe mkoani Kigoma,"amesema.
Dk.Kalemani amesema gharama za utekelezaji wa mradi ni Dola za Marekani milioni 150.0 sawa na takriban Sh. bilioni 346.30. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na kukamilisha: Upembuzi Yakinifu wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 29 132; usanifu (design) wa miundombinu ya mradi; upimaji na uthamini wa eneo la mradi na njia ya kusafirisha umeme; na mpango wa kuhamisha wananchi wanaopisha mradi. 32.
Ameweka wazi katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kutwaa ardhi na kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; kumpata Mtaalam Mshauri na Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi na njia ya umeme msongo wa kV 132. Jumla ya Shilingi bilioni 3 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi milioni 600 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.40 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuanza Septemba, 2020 na kukamilika Septemba, 2023.
Amesema Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kikonge – MW 300 33, unahusu ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha umeme wa MW 300 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhuhu mkoani Njombe na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 132 yenye urefu wa kilomita 53 kutoka Kikonge hadi kituo 30 cha kupoza umeme cha Madaba. Gharama za utekelezaji wa mradi zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani Milioni 750 sawa na takriban Shilingi trilioni 1.737. Mradi huu pia unahusisha upatikanaji wa maji kwa ajili ya umwagiliaji.
"Kazi zilizotekelezwa kwa mwaka 2018/19 ni kumpata Mtaalamu Mshauri wa kufanya Upembuzi Yakinifu (Feasibility Study) na Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira na Kijamii (Strategic Environmental & Social Assessment – SESA). Kazi hizi zinafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).Katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kukamilisha Upembuzi Yakinifu pamoja na Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira na Kijamii (SESA); kukamilisha majadiliano ya ufadhili wa ujenzi wa mradi na kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 2.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi milioni 500 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2 ni fedha za nje.
"Mradi huu unatarajiwa kuanza Novemba, 2020 na kukamilika Oktoba, 2023. 31 Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Murongo/Kikagati – MW 14 35. Mradi huu wa nchi mbili za Tanzania na Uganda unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 14 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera na ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kV 33 yenye urefu wa kilomita 0.7 kutoka Kikagati (Uganda) hadi Murongo (Tanzania).
"Mradi utagharimu Dola za Marekani milioni 58 ambazo ni takriban Shilingi bilioni 134.35 na unatekelezwa na mwekezaji binafsi, Kampuni ya Kikagati Power Company Ltd (KPCL). 36. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: kukamilisha ujenzi wa kambi ya kudumu ya wafanyakazi na miundombinu ya barabara za kuingia eneo la mradi; usanifu wa mitambo na vifaa ya umeme; na ujenzi wa miundombinu ya kukinga na kuingiza maji (Dam and Intake) na njia za kupitisha maji (waterways).
"Kazi zitakazotekelezwa kwa mwaka 2019/20 ni pamoja na: kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya kuzalisha umeme; na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 33. Mradi huu ulianza mwezi Novemba, 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2020. 32 Matengenezo ya Mtambo wa Kuzalisha Umeme wa Hale (Rehabilitation of Hale Hydro Power Plant) – MW 21 37. Mradi huu unahusu uboreshaji wa mifumo ya uendeshaji na ukarabati wa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia maji wa Hale mkoani Tanga.
" Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa SEK milioni 200 ambazo ni takriban Shilingi bilioni 50.96 zitakazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Sweden kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (Sida). Kazi zilizofanyika katika mwaka 2018/19 ni kukamilisha taratibu za kumpata Mkandarasi wa ukarabati wa mitambo. 38. Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni pamoja na kuanza uchimbaji wa handaki la kuingia katika kituo cha kuzalisha umeme (access tunnel).
"Jumla ya Sh.bilioni 7.80 zimetengwa kutekeleza kazi hizo ambapo kati ya fedha hizo Shilingi milioni 300 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 7.50 ni fedha za nje. Kazi za ukarabati zinatarajiwa kuanza mwezi Agosti, 2019 na kukamilika ifikapo mwezi Desemba, 2021. 33 Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi II – MW 240 39. Ujenzi wa mradi huu ulianza Machi, 2016 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 344, sawa na takriban Sh.bilioni 794.12,"amesema.
Akielezea zaidi mradi huo amesema ulihusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 240 kwa kutumia gesi asilia katika eneo la Kinyerezi Jijini Dar es Salaam. Kituo hiki chenye jumla ya mitambo nane (8), ambapo mitambo sita (6) ni ya kutumia gesi asilia (gas turbines) na mitambo miwili (2) ni ya kutumia mvuke (steam turbines) kilikamilika na kukabidhiwa rasmi kwa TANESCO mwezi Desemba, 2018. Kukamilika kwa kituo hiki kumeongeza jumla ya MW 248.22 katika Gridi ya Taifa.
Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi I Extension – MW 185 na kwamba mradi huo upo katika hatua za mwisho za utekelezaji unahusu upanuzi wa kituo cha Kinyerezi I – MW 150 kwa kuongeza mitambo itakayozalisha MW 185 na kufanya kituo hicho kuzalisha jumla ya MW 335. Mradi 34 huu unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 188 sawa na takriban Shilingi bilioni 435.48. Katika mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: kukamilika kwa utengenezwaji wa mitambo yote minne (4)
Na kuanza kufungwa katika eneo la mradi; kukamilika kwa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kinyerezi I kV 220 na kuendelea na upanuzi (upgrade) wa njia ya msongo wa kV 132 kutoka Kinyerezi I hadi kituo cha kupoza umeme cha Gongo la Mboto. Ujenzi wa mradi huu ulianza mwezi Juni, 2016 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2019. 41. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2019/20 kazi zitakazotekelezwa ni kukamilisha ufungaji wa mitambo na kuingiza jumla ya MW 185 katika Gridi ya Taifa. Fedha za ndani Shilingi bilioni 60.00 zimetengwa katika mwaka 2019/20 kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo.
"Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Mtwara – MW 300, mradi huu unahusu ujenzi wa mitambo ya kuzalisha MW 300 kwa kutumia gesi asilia katika Mkoa wa Mtwara. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 360 sawa na takriban Shilingi bilioni 833.90. Mradi huu utatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA) kwa kushirikiana na Serikali. Kazi zilizofanyika katika mwaka 2018/19 ni pamoja na: kukamilika kwa Upembuzi Yakinifu wa kituo cha kuzalisha umeme na miundombinu wezeshi ya maji, barabara na gesi asilia.
"43. Katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na kukamilisha uthamini na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi; kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; na kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 4.20 zimetengwa katika mwaka 2019/20 kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Sh. bilioni 1.00 ni fedha za ndani na Sh.bilioni 3.20 ni fedha za nje. Mradi 36 huu unatarajiwa kuanza mwishoni mwa Machi, 2020 na kukamilika Septemba, 2022
" Miradi ya Kufua Umeme Utokanao na Jua – MW 150, Upepo – MW 200 na Makaa ya Mawe – MW 600 , Septemba 2018, Serikali kupitia TANESCO ilitangaza miradi ya nishati jadidifu (Jua – MW 150 na Upepo – MW 200) na Makaa ya Mawe – MW 600 kwa wawekezaji binafsi. Lengo ni kupata miradi ya kuzalisha umeme wa jumla ya MW 950 kwa njia ya ushindani na kuingizwa katika Gridi ya Taifa. Hadi kufikia mwezi Februari, 2019 tathmini ya zabuni kwa kampuni zilizoshiriki ilikamilika,"amesema.
Ameongeza taratibu zinazoendelea kwa sasa ni kampuni zilizopita hatua ya awali kuwasilisha mapendekezo ya namna bora ya kuendeleza miradi husika baada ya kupatiwa Request for Proposals (RFPs) na kwamba katika kipindi cha mwaka 2019/20, TANESCO itakamilisha taratibu za kuwapata wawekezaji binafsi wenye bei nafuu na kuanza utekelezaji wa miradi hiyo. Utekelezaji wa miradi hii nafuu utapunguzia Shirika gharama za uendeshaji 37 na hivyo kuwepo matarajio ya kushuka kwa bei ya umeme. Utekelezaji huo unatarajiwa kuanza mwezi Novemba, 2019 na kukamilika mwezi Oktoba, 2022.
MIRADI YA KUSAFIRISHA UMEME
Dk.Kalemani ametumia nafasi hiyo kuelezea Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 wa Singida – Arusha – Namanga ambapo amsema mradi huo unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 414 kutoka Singida hadi Namanga kupitia Arusha. Pia unahusisha ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme katika eneo la Kisongo mkoani Arusha, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme (bay addition) cha Singida na usambazaji wa umeme katika vijiji 22 vinavyopitiwa na mradi. Mradi unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na Serikali ya Tanzania. Gharama ya mradi ni Dola za Marekani milioni 258.82 sawa na takriban Shilingi bilioni 599.53. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni kulipa fidia na kuanza shughuli za ujenzi wa mradi. 38 47.
"Kazi zilizopangwa kufanyika kwa mwaka 2019/20 ni: kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 4 fedha za nje zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Utekelezaji wa mradi huu ulianza mwezi Machi, 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2020. 48. Utekelezaji wa mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Backbone awamu ya pili (Backbone Phase II) unaohusu kuongeza uwezo (upgrade) wa vituo vya kupoza umeme kutoka kV 220 mpaka kV 400 katika mikoa ya Iringa na Shinyanga kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na katika mikoa ya Singida na Dodoma kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA).
"Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 kutoka Makambako hadi Songea na Kusambaza Umeme Vijijini kwa Mikoa ya Njombe na Ruvuma 49. Mheshimiwa Spika, mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa 39 kV 220, yenye urefu wa kilomita 250 kutoka Makambako hadi Songea kupitia Madaba pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Madaba na Songea na upanuzi wa kituo cha Makambako ulianza mwezi Mei, 2016 na kukamilika mwezi Septemba, 2018.
"Mradi huu ulizinduliwa rasmi na Rais Dk. John Magufuli Aprili 6, 2019. Hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2019 jumla ya vijiji 112 kati ya 122 vilikuwa vimeunganishwa umeme. Jumla ya wateja wapatao 22,700 wanatarajiwa kuunganishwa umeme kupitia mradi huu katika wilaya za Makambako, Njombe na Ludewa katika Mkoa wa Njombe; na Songea Vijijini, Songea Mjini, Namtumbo na Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma. Gharama ya mradi huu ilikuwa ni Shilingi bilioni 216 chini ya ufadhili wa Serikali za Tanzania na Sweden,"amesema.
Amefafanua kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni: kuendelea kuunganisha wateja ikiwemo Vijiji vya Lutikila, Ifinga na Mbangamawe mkoani Ruvuma vilivyoongezeka pamoja na kukamilisha kazi ya kufunga Reactor na Distribution Panels katika vituo vya kupoza 40 umeme vya Makambako, Madaba na Songea. Jumla ya Shilingi bilioni 2.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Sh.bilioni 2 ni fedha za ndani na Sh. milioni 500 ni fedha za nje.
"Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 Bulyanhulu – Geita 51. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi ni kujenga njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 55 kutoka Bulyanhulu hadi Geita. Mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Geita kV 220, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Bulyanhulu, usambazaji wa umeme katika vijiji 10 vilivyopo ndani ya eneo la mradi na kubadilisha mita za umeme za kawaida (conventional meters) 1,500 mkoani Geita. Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 23 sawa na takriban Shilingi bilioni 53.28. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni kupatikana kwa Mkandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme; kuanza ujenzi wa kituo cha kupoza umeme; kupatikana kwa Mkandarasi wa usambazaji umeme vijijini; na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi,"amefafanua.
Ameeleza kuwa kazi zitakazofanyika mwaka 2019/20 ni kukamilisha: ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme mkoani Geita; upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Bulyanhulu; ujenzi wa njia za kusambaza umeme za msongo wa kV 33 na kV 0.4 katika vijiji 10; na kuunganisha wateja wapya 1,500. Jumla ya Sh.bilioni 4.10 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Sh.bilioni 1.50 ni fedha za ndani na Sh.bilioni 2.60 ni fedha za nje.
Dk.Kalemani amesema ujenzi wa mradi huo ulianza Januari, 2019 na unatarajiwa kukamilikaMei, 2020. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Geita – Nyakanazi na kwamba unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 133, kituo cha kupoza umeme Nyakanazi na kusambaza umeme katika vijiji 32 vinavyopitiwa na mradi.
Ambapo gharama za utekelezaji wa mradi huu ni EURO milioni 45 sawa na takriban Shilingi bilioni 117.79. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni: kukamilisha upatikanaji wa Mkandarasi; 42 kukamilisha uhakiki wa mali za wananchi watakaopisha mradi na kuanza kulipa fidia.Kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni kuanza: ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Geita hadi Nyakanazi; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi; upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Geita kitakachojengwa kupitia Mradi wa Bulyanhulu – Geita; na usambazaji wa umeme katika vijiji 32. Fedha za nje Shilingi bilioni 1 zimetengwa katika mwaka 2019/20 kwa ajili ya kazi hizo.
"Ujenzi wa mradi huu utaanza Agosti, 2019 na kukamilika mwezi Julai, 2021. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 Rusumo – Nyakanazi 55. Mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 98.2 kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha Rusumo hadi Nyakanazi. Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 35 sawa na takriban Sh. bilioni 81.07. Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Tanzania,"amesema.Hotuba kamili inapatikana katika tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.nishati.go.tz.
Waziri wa Nishati Dk.Medrard Kalemani akiwasilisha makadirio ya bajeti ya fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2019/2020 bungeni Mjini Dodoma leo
Sehamu ya viongozi wa Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zake wakifuatilia hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizata ya Nishati kwa mwaka 2019/2020 ambayo imewasilisha leo Bungeni Mjini Dodoma
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza Bungeni wakati wa Wizara hiyo ikiwasilisha makadirio ya bajeti yake kwa mwaka 2019/2020
Mbunge wa Muleba Kaskazini akichangia hotuba ya bajaeti ya Wizara ya Nishati ambayo imewasilisha leo Bungeni Mjini Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...