Na Theresia Malya, Afisa Habari Tunduru
Benki
ya posta Tanzania Tawi la Tunduru imekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi
milioni 2,949,000.00 kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru kwa ajili
ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi vyenye wa ngozi waliopo katika shule za
msingi na sekondari wilayani Tunduru.
Akikabidhi
vifaa hivyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Ndg Gasper Balyomi Meneja wa Benki ya Posta
tawi la Tunduru Bi. Emajackline Mtemba alisema vifaa hivyo ni mafuta kinga,
kofia za kujikinga na mionzi ya jua
(pama), Miwani, Sabuni za kuoga, na Viookuza (Magnifier).
Bi
Mtemba aliwaasa watoto hao kutumia vifaa hivyo kusoma vizuri na view chachu ya
kuongeza bidii katika masomo yao,kuweni na
nidhamu kwa kutii wazazi na
walimu “lakini vifaa hivi viwe chachu kwenu ya kusoma na kufanya vizuri Zaidi
kwenye masomo yenu kwani nyie ndio viongozi wa baadaye na ni matarajio ya benki
ya posta ya Tanzania kuwa watoto hawa wenye ulemavu wa ngozi wana nafasi kwenye
jamii kama walivyo watoto wengine na ndio viongozi wa baadaye”
Nitoe
wito kwa wazazi wote kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu wa ngozi
kwani wao wana haki ya kupata elimu kwani ni haki ya msingi kwa kila mtoto na
serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inawatambua na kuwajali, pia
niwakumbushe wazazi kuwawekea watoto Amana kwa ajili ya kusomea ili kuondoa
changamoto ya ukosefu wa Ada.
Akitoa
taarifa fupi ya Halmashauri ya Tunduru mgeni
rasmi ambaye pia Mkurugenzi Mtendaji Ndg.
Gasper Zahaoro Balyomi alianza kwa kuishukuru benki ya posta Tanzania tawi la Tunduru kutoa vifaa saidizi kwa watoto
wenye ulemavu wa ngozi wilayani Tunduru ambapo alipokea kofia 72, mafuta kinga
chupa 72, sabuni 72, miwani na viookuza kwa ajili ya kugawa kwa wanafunzi hao.
Gasper
Balyomi aliendelea kusema Halmashauri ya Tunduru ina shule 149 za serikali kati
ya hizo ndio zilizo na vitengo vya elimu
maalum, ambazo ni Tunduru Mchanganyiko na
Namiungo shule ya Msingi.
“Tunduru
ina shule za msingi 149 za serikali na shule mbili za Namiungo na Tunduru
Mchanganyiko ndio wanapokea watoto wenye mahitaji maalum, lakini ina idadi ya
wanafunzi wenye ulemavu 432 ikiwa
wasichana ni 167 na wavulana 265, na upande wa shule za sekondari ina wanafunzi
27, wasichana 12 na wavulana 15, lakini watoto wenye ulemavu wa ngozi ni 36
ikiwa wasichana ni 19 na wavulana 17”alisema Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Tunduru.
Aidha
alisema changamoto kubwa wanayokumbana nayo watoto hawa wenye ulemavu wa ngozi
ni pamoja na kukosekana kwa mafuta kinga, miwani, kofia za kujikinga na mionzi
ya jua (Pama), lakini pia kukosekana kwa huduma za matitabu ya ngozi katika
hospitali za wilaya na badala yake zinapatikana katika hospitali zenye vitengo maalumu
kama hospitali KCMC iliyopo Moshi, Bugando mwanza na Muhimbili ambapo wazazi
wanashindwa kumudu gharama za kuwasafirisha watoto hawa.
Aliendelea
kutanabaisha kwa kusema Halmashauri ina walemavu wa aina mbalimbali
hivyo ni vyema jamii na wadau wa maendeleo kujitokeza katika kuwawesha ili
waweze kusoma na kufikia malengo yao kwani miongoni mwa hawa watoto wapo wenye
vipaji ambavyo vinahitaji kuendelezwa.
Mkurugenzi
huyo alisema kuwa Halmashauri ina mpango mkakati wa kuanzisha ya shule ya watoto wenye mahitaji
maalum kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari ambao wakifaulu wanashindwa
kuendelea na masomo.
Sambamba
na kuanzishwa kwa shule hiyo lakini kwa sasa tuna mikakati ya kuiombea shule
ya sekondari Nandembo iliyopo wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma kuanzisha kitengo cha Elimu maalum ili kupunguza
changamoto ya wanafunzi wanaofaulu kuendelea na masomo ya juu kutumia nafasi
zao kwani wengi wanashindwa kwenda shule wanazopangiwa nje ya wilaya kutokana
na wazazi kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya Halmshauri ya Tunduru Kaimu afisa elimu Bi Loya Mwajabu
kwa Benki ya Posta Tawi la Tunduru alisema
serikali kupitia sera ya elimu ya
mwaka 2004 haijabagua watoto kwani watoto wote ni sawa na wanatakiwa kupata
elimu kwani ni haki ya msingi.
Alisema
Kupata elimu kwa watoto kutamsaidia mtoto kujitambua na kupata urithi ulio
sahihi, mama ni mlezi mkubwa na nikuhakikishie kuwa hawa watoto watatumia vifaa
hivi vile iliyoelekezwa, wito wetu kwa jamii ni kuwa hawa wamezaliwa hivi walivyo na wana haki ya
kupata elimu kwani ndio ukombozi wao.
Aidha
niwaombe wazazi, jamii na wadau wa elimu
na maendeleo ndani nan je ya wilaya ya Tunduru kuguswa na watoto hawa, kuunga
mkono juhudi za serikali katika
kuwasaidia vifaa saidizi watoto kwani watoto 432 wenye ulemavu ni wengi
sana na sio hawa wenye ulemavu wa ngozi tuu,pia wapo wenye mtindio wa ubongo,
bubu viziwi, viwete na wote hawa wanahitaji kusaidiwa kufikia ndoto zao.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru Ndg Gasper Balyomi akimvisha kofia
ya kujikinga na mionzi ya jua (pama) wakati alipokua akipokea vifaa kutoka kwa
meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduru Bi.Emajackline Mtemba vyenye thamani Tsh 2949,000.00 katika halfa
iliyofanyika ukumbi wa Klasta..
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru Ndg Gasper Balyomi akiongea katika hafla ya kupokea vifaa kutoka kwa meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduru Bi.Emajackline Mtemba vyenye thamani Tsh 2949,000.00 katika halfa iliyofanyika ukumbi wa Klasta..
Meneja wa benki ya posta Tanzania tawi la
Tunduru Bi Emajackline Mtemba akiongea na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi,
wazazi na walimu wakati alipokuwa akikabidhi vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye
ulemavu wa ngozi wilayani Tunduru iliyofanyika katika ukumbi wa Klasta
Mlingoti.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Gasper Zahoro Balyomi akikabidhi vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wilayani Tunduru vilivyotolewa na benki ya Posta tawi la Tunduru
Meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduru
Bi.Emajackline Mtemba akikabidhi vifaa saidizi kwa ajili ya watoto wenye
ulemavu wa ngozi vyenye thamani ya
Tsh.2,949,000.00 kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru Ndg Gasper
Zahoro Balymi kwenye halfa iliyofanyika ukumbi wa Klasta Tunduru.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...