Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa ameitaka Taasisi ya Watumishi Housing Company (WHC) kujitangaza kwa Watumishi wa Umma, Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Wananchi ili kupata wateja kwenye Mradi wa Nyumba uliopo Gezaulole, Kigamboni na Bunju B jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada yakutembelea miradi ya ujenzi wa Nyumba hizo zinazosimamiwa na Watumishi Housing, Dkt. Mwanjelwa amesema WHC inapaswa kujitangaza kwa wateja ambao ni Watumishi wa Umma na Watanzania ili kujua kuhusu Nyumba hizo bei zake, pamoja na mandhari ya nyumba hizo. 

"Kila kizuri mnachokifanya Watanzania watajuaje?, Taasisi hii ipo Kisheria, Kikatiba, lazima mseme msikike kwa Watanzania, Watumishi wa Umma wajue mandhari,  waweza kujipanga kuweza kumudu gharama za Nyumba hizo," amesema Dkt. Mwanjelwa

"Sehemu kama Dodoma, Gezaulole Kigamboni kuna miradi mikubwa ya Nyumba, jitahidini kutangaza miradi hiyo", ameongeza Dkt. Mwanjelwa 

 Kuhusu suala la Wakandarasi, Dkt. Mwanjelwa amehoji uwepo wa Wakandarasi wanne katika mradi huo, ambapo amesema hakuna haja yakuwa na wingi huo ili kupunguza gharama, ameomba Kampuni ya Watumishi Housing kusimamia zaidi mradi huo. 

Pia Dkt. Mwanjelwa amewata WHC kufanya vizuri zaidi kuboresha mapungufu yote kwenye miradi hiyo, ili kupata matokeo mazuri kwa kutumia ubunifu waliokuwa nao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC) , Dkt. Fredy Msemwa ameahidi kuyafanyia kazi maagizo na maelekezo ya Naibu Waziri nakurejesha mrejesho uliokuwa wazi, amesema watakaa chini kurejea upya mkakati wa Elimu kwa Umma na Masoko katika kujitangaza ili kukidhi matarajio ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

"Sisi kama Taasisi tutakaa chini kurejea vizuri mkakati wetu mpya wa Elimu ya Umma na Masoko ili kukidhi matarajio yako wewe Naibu Waziri na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora tukiweza kufanya hivyo tutakuwa tumefikia matarajio ya Serikali, cha muhimu zaidi ni Watumishi wa Umma na Walengwa wengine kuweza kujua uwepo wa mradi wa Nyumba hizo, "amesema Dkt. Fredy

Amesema WHC tayari imefika kwenye Mikoa 16 hapa nchini sehemu ngumu kwenye ujenzi wa Shule za Kata zenye mazingira magumu, amesema wamewafikia Watumishi wa Umma kwa bei nafuu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa (kulia) akizungumza jambo na   Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa wakati wa ziara ya kutembelea mradi ya ujenzi wa nyumba wa Gezaulole, Kigamboni jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Emmanuel Mssaka wa Michuzi Tv)
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa  (katikati) akiwa ameambatana na watendani mbalimbali  wakitembelea Miradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea miradi ya nyumba zilizopo Gezaulole, Kigamboni na Bunju B jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya  kutembelea miradi ya nyumba zilizopo Gezaulole, Kigamboni na Bunju B jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa majengo ya Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa majengo ya Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. 


Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa barabra katika  Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Emmanuel Mssaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...