Naibu Waziri Ofisa ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka (kulia), alipokwenda kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa wa DCB jijini Dar es Salaam. Kushoto nyuma ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (katikati).

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemeni Jafo amesema Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kuweka mazingira  wezeshi ya uwekezaji na biashara kwa kuhuwisha sera na sheria. Jafo amesema kwamba lengo la kufanya hivyo ni kuendelea  kuvuta wawekezaji katika taasisi za fedha nchini Tanzania na hasa kuwekeza kwenye mabenki.

Amesema hayo wakati anafungua Mkutano Mkuu wa 17 wa mwaka wa wanahisa wa benki ya DCB jijini Dar es Salaam. Akizungumza kwa niaba ya Waziri Jafo, Naibu Waziri wa TAMISEMI Josephat Kandege amesema Serikali imekua  ikieweka mazingira mazuri kwa ajili ya uwekezaji nchini na itaendelea kufanya hivyo.

Ametoa mwito kwa halmashauri zote nchini kununua hisa za benki hiyo kwani mbali ya kupata faida watanufaika na uzoefu ambao benki hiyo wanao hasa wa kushirikiana na manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam katika uendeshaji wa mitaji ya kifedha na usimamizi bora wa fedha.

Akifafanua zaidi wakati akisoma hotuba ya Jafo,Naibu Waziri Kandege amesema kwa nyakati tofauti TAMISEMI imekuwa ikitoa maelekezo kwa halmshauri nyingine ziige mfano wa Manispaa za Dar es Salaam kwa kununua hisa za benki hiyo na kimsingi ndio chimbuko la kuanzishwa kwa benki hiyo.
Pia ametoa pongezi kwa bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo, menemejimenti na wafanyakazi wote kwa mafanikio makubwa waliyonayo na kuifanya benki hiyo kuwa ya mfano.

"Pia nitoe pongezi kwa kufanisha mchakato wa kuuza hisa kiasi cha kuvuka lengo lenu.Ni jambo nzuri pia  kuorodheshwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam.Kwa kufanya hivyo mnatoa fursa kwa wananchi na wawekezaji kwa ujumla kuendelea kunufaika na benki hii,"amesema.

Ameongeza TAMISEMI inafarijika kuona mshikamano uliopo kati ya wanahisa waanzilishi, wanahisa wapya na wawekezaji wengine kwa ujumla na kuongeza kufika kwao kwenye mkutano huo ni kielelezo tosha wana nia ya adhati kuwekeza katika benki yao kwa lengo la kukuza mtaji wake na kupata faida.

Ameongeza manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo alisema kimsingi ndiyo wamiliki wake wakubwa wametoa mchango mkubwa katika kufikia mafanikio hayo.  

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Profesa Lucian Msambichaka amesema mchakato wa uuzwaji hisa za benki hiyo na hatimaye kuorodheshwa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), ni ishara kuwa benki hiyo  ina mvuto na inafanya kazi vizuri.

Wakati Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa amewahakikishia wanahisa wa DCB kuwa benki yao itaendelea kufanya vizuri kutokana na mikakati waliyojiwekea.


Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam ambazo ndio wanahisa wakubwa wa benki hiyo, wana imani kubwa na utendaji wake na kuongeza uongozi wa benki hiyo wamekuwa wakifanya mabadiliko makubwa yenye tija kubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...