Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Washiriki wa Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya St. Gaspar, jijini Dodoma, leo. Lugola aliwataka washiriki hao ambao ni Wanasheria kutoka Wizara mbalimbali, Taasisi za Serikali pamoja na Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS) kufanya maboresho ya Mfumo huo kwa lengo la kuleta mipango yenye manufaa Serikalini kwa maendeleo ya nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimsalimia Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika Ukumbi wa St. Gaspar, jijini Dodoma, leo, kwa lengo la kuzungumza na Washiriki wa Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai ambao ni Wanasheria kutoka Wizara mbalimbali, Taasisi za Serikali pamoja na Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS) wapo katika mkutano wa kuboresha mfumo huo. Lugola aliwataka washiriki hao kuleta mipango yenye manufaa Serikalini kwa maendeleo ya nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome wakati alipokuwa anazungumza na washiriki wa Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai ambao ni Wanasheria kutoka Wizara mbalimbali, Taasisi za Serikali pamoja na Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS), katika Ukumbi wa St. Gaspar, jijini Dodoma, leo. Katika mkutano huo, Lugola aliwataka washiriki hao kuleta mipango yenye manufaa Serikalini kwa maendeleo ya nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitumia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwafafanulia jambo Washiriki wa Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai, jinsi Ilani hiyo inavyofanya kazi bega kwa bega na Sheria za nchi ikiwemo katika maboresho hayo ya mfumo wa haki jinai. Waziri Lugola aliwataka washiriki hao kuleta mipango yenye manufaa Serikalini kwa maendeleo ya nchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
……… 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola amekitembelea kikosi kazi kinachopitia mfumo wa haki jinai nchini ili kuufanyia maboresho na kukitaka kuangalia kwa umakini maeneo yote ambayo yamekuwa changamoto na kuwafanya wananchi kukosa haki zao. 

Mhe. Lugola ametoa kauli hiyo alipotembelea kambi maalum ya wataalamu wa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo iko jijini Dodoma kwa ajili ya kuupitia mfumo wa haki jinai nchini na kuangalia changamoto inazoukabili mfumo huo ili kuufanyia maboresho. 

“Nimekuja hapa kuangalia kazi mnayoifanya ila nataka niwaambie kwamba muangalie kwa makini maeneo yote katika mfumo wa haki jinai ambayo yamekuwa yakiwanyima haki wananchi na hata kufanya haki za binadamu kuvunjwa,” amesema 

Mhe. Lugola amewataka wataalamu wanaofanya kazi hiyo ya maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini kuangalia namna ya mashauri yanayoweza kupata dhamana, muda wa kuendesha mashauri ya watuhumiwa na aina za adhabu zinazotolewa ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati kwani haki inayocheleweshwa ni sawa na kunyimwa haki. 

Pia amewataka kuangalia, namna ya kukabiliana na rushwa kubwa na mabadiliko ya sayansi na teknolijia ambayo yamesababisha kuongezeka kwa mbinu za uhalifu na hivyo kuuacha nyuma mfumo wa haki jinai nchini. 
Amesema wazo la kuufanyia maboresho mfumo wa haki jinai litawezesha mfumo huo kwenda na wakati na kutoa haki kwa wananchi huku haki za binadamu zikizingatiwa. 

Ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa kukutanisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na nje ya serikali ili kufanya maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini na kumtaka Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome kufikisha salamu kwa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Augustine Mahiga kwa kuja na mpango wa kuufanyia maboresho mfumo wa haki jinai nchini na kwamba kitendo hicho ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala cha CCM . 

“Katibu Mkuu niwapongeze sana na nikuombe umfikishie salamu za pongezi mhe Waziri Dkt. Mahiga, kitendo cha kuufanyia maboresho mfumo wa haki jinai ni cha kupongezwa, kimekuja wakati na kinatekeleza kwa vitendo ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020,” amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...