Na, Editha Edward-Tabora 

Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Sikonge Umepewa mwezi mmoja kuhakikisha unakamilika Ujenzi wa majengo saba ya Hospitali ya wilaya ili kuweza kutoa huduma kama ilivyokusudiwa 

Agizo limetolewa na Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri katika Ziara yake ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo ambayo ilipaswa  kukamilika Mwishoni mwa mwezi juni mwaka huu

Mwanri amesema hadi kufikia sasa majengo mawili hayajaezekwa jambo ambalo linaonesha kuwa haitawezekana kukamilisha kwa wakati na kuhakikisha wamerekibisha kasoro zote zilizojitokeza katika jengo la Utawala na la wagonjwa wa nje ( ODP)  na kuweka mfumo wa maji kabla ya kuendelea na Ujenzi 

Amesema ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeagiza kuwa kila Halmashauri iliyopatiwa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Hospital ya wilaya kuhakikisha Ujenzi unakamilika juni 28 mwaka huu lakini  kwa kasi ya sikonge haiwezi kukamilisha ndani ya kipindi walichopangiwa 

Mkurugenzi mtendaji  wa Halmashauri ya wilaya ya sikonge Martha Luleka amesema kuwa wameshindwa kukamilisha majengo kwa wakati kwasababu ya baadhi ya mafundi waliokuwa wamewapa Kazi waliwabaini kuwa utendaji Kazi wao siyo mzuri hivyo kulazimika kuvunja nao mkataba

Pia amemalizia kwa kusema Sababu nyingine ni wizi wa vifaa vya Ujenzi unaosababisha hadi kufikia sasa jumla ga Shilingi bilioni 1.168 zimetumika katika Ujenzi wa majengo saba ya hospital ya wilaya hiyo

Hata hivyo Halmashauri ya wilaya ya Sikonge ilipokea bilioni 1.5 kwa ajili ya Ujenzi wa hospital ya wilaya ambapo hadi sasa zimetumika Shilingi bilioni 1.1.
Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza na wananchi wa Sikonge.
 Pichani ni Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akikagua maendeleo ya Ujenzi wa hospital ya Wilaya ya sikonge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...