Ili kupunguza umaskini kwa mwananchi mmoja mmoja na kuwainua kiuchumi halmashauri ya mkuranga kwa kushirikiana na wizara ya mifugo na uvuvi imeendesha mafunzo ya siku moja ya ufugaji kwa wafugaji wa wilaya hiyo yatakayo wawezesha kujitegemea kiuchumi,na kufanya nchi iweze kufikia uchumi wa kati wa viwanda.


Akifungua mafunzo hayo leo katika ukumbi wa Flex Hotel Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Hamisi Ulega(Mb) aliwataka washiriki wawe watulivu na wasikivu na kuwa mabalozi wa nzuri kule waendapo.

Aidha Ulega aliwataka wananchi wa Wilaya ya Mkuranga kuyatumia mafunzo hayo ya ufugaji wa kisasa vizuri ili yalete tija na hatimaye wajikwamue kiuchumi sambamba na kupaisha mapato ya Halmashauri ya Wilaya na nchi kwa ujumla.

Ulega pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina kwa kuichagua wilaya hiyo ambayo yeye ni Mbunge kutoa elimu ya ufugaji bora. “Nawaomba mtumie fursa hii vizuri kujikwa mua kiuchumi na yasiishie hapa mkawape elimu na wengine.” Alisema ulega

“Naomba niwaambie mafunzo haya hatujaanza kutoa hapa tumeshatoa katika Wilaya mbili ikiwemo Simanjiro mkoani Manyara na Kaliuwa Mkoani Tabora lengo ni kutoa elimu na kuwajengea uwezo wananchi juu ya ufugaji bora wa kisasa.”alisema

Hata hivyo ulega aliwataka wananchi kujikita kwenye ufugaji kama mbadala wa kilimo cha korosho , huku akishukuru wizara kwa kuichagua wilaya hiyo kuwa kituo cha uksanyaji maziwa kwa kanda sambamba na kiwanda cha chakula cha mifugo ambacho malighafi yake ni mihogo.

Alisema kituo hicho cha ukusanyaji wa maziwa kitakuwa na uwezo wa ukusanyaji wa maziwa kuanzia lita elfu tano mpaka elfu kumi kwa siku hivyo ametoa wito kwa wananchi kufuga kwani soko lipo

Hata hivyo Ulega amewatoa hofu wananchi kuhusu mtaji na kusema kuwa wilaya imejipanga vizuri wanachotakiwa ni kuunda vikundi ili waweze kupatiwa mikopo kwani kuna fursa nyingine ya ujio wa Benki ya kilimo ambayo itakopesha vikundi vya wafugaji na wavuvi kwa masharti nafuu

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mhandisi Mshamu Munde alishukuru ujio wa wataalamu toka wizarani hiyo akiweka bayana viwango vya ardhi ya kutosha vilivyopo katika halmashauri hiyo kwa ajili ya viwanda mbalimbali vinavyotoa fursa kwa wakulima na ufugaji.

Akizungumza wakati wakufunga mafunzio hayo Mkuu wa wilaya ya Mkuranga,Filbeto Sanga alisema anaishukuru wizara kwa kuleta mafunzo hayo kwani inawezekana ikawa muorobaini wa wafugaji kahamhama na kupunguza migogoro ya wakulima na wafuaji katika wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega(Mb)akizungumza na waanchi wa wila ya Mkuranga leo wakati wa kufungua mafunzo ya ufugaji bora yaliyo fanyika katika ukumbi wa Flex Wilayani Mkuranga mkoani Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkufanga, Mhandisi Mshamu Munde akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo ambapo alishukuru ujio wa wataalamu toka Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwa kutowa mafunzo ya ufugaji bora.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega(Mb) akisaliamina na wananchi,viongozi na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani mara baada ya kuwasali katika ukumbi wa Flex kwa ajili ya kufungua mafunzo ya ufugaji bora.
Mratibu wa Dawati la sekta Binafsi kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi,Stephen Michael akifafanua jambo katika mafunzo ya ufugaji bora aliyo fanyika katika ukumbi wa Flex Hotel Wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Baadhi ya wananchi na viongozi na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani wakimsikilza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah 

Ulega(Mb) hayupo pichani alipo kuwa akufungua mafunzo ya ufugaji bora yaliyo fanyika katika ukumbi wa Flex leo Wilayani Mkuranga mkoani Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...