Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio za siku mbili katika halmashauri mbili za wilaya ya Arumeru ambapo jumla ya miradi 15 Kati ya Miradi 16 yenye thamani ya Bilioni 22.9 imezinduliwa, kuwekewa mawe ya msingi, na mingine kukaguliwa na kuangalia uendelevu wake
Akihitimisha mbio hizo za mwenge kwa halmashauri ya Meru , kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019 Ndugu Mzee Mkongea Ali mbali na kuridhishwa na ubora wa miradi ,amempongeza Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro kwa kuisimamia vizuri na kuhakikisha miradi hiyo inaleta tija kwa taifa
Akizungumza katika mradi wa Maji wa Majengo wenye thamani ya shilingi milioni 754 ambao ulipaswa kuwekewa jiwe la msingi , kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Mzee Mkongea Ali amesema mradi huo japo ni mzuri na umefikia katika hatua nzuri na kuanza kutoa huduma
Aisha ameitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU kuchukua hatua kali kwa aliekuwa mhandisi wa maji wa Halmashauri ya Meru ambae amehamishwa kwa kuidhinisha malipo ya shilingi milioni mbili(2,000,000)ambayo hayakufanya kazi iliyokusudiwa
Mkuu wa wilaya ya Arumeru amemshukuru Kiongozi wa mbio za mwenge 2019 pamoja na wakimbiza mwenge wengine ambapo amewahidi kuongeza kasi ya usimamiaji wa miradi mingine ambayo haikuwepo kwenye ratiba za mwenge ili pamoja nayo iweze kukamilika mapema na kuleta tija kwa taifa
Mwenge wa uhuru umendelea na mbio zake katika wilaya ya Arusha Jiji , kisha utakwenda Monduli na kumaliza mbio zake karatu kabla ya kukabidhiwa kwa mkoa wa Manyara siku ya Alhamisi
Picha Kiongozi wa mwenge kitaifa Mzee Mkongea Ally akiwa na mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakipitia moja ya jalada la mradi wa majengo ambao mradi huo upo vyema lakini kiasi cha shilingi milioni 2kimetumika ndivyo so ndivyo sivyo.

Kiongozi wa mwenge kitaifa Mzee Mkongea Ally akiwa na mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakipitia moja ya jalada la mradi wa majengo ambao mradi huo upo vyema lakini kiasi cha shilingi milioni 2kimetumika ndivyo so ndivyo sivyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...