Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

MKURUGENZI wa Kampuni ya Biabana Anna Kristina Edler, (54) na mumewe Anders Svensson 58 wamefanikiwa kulipa faini ya Sh.milioni 20 kwa kila mmoja na hivyo kukwepa kifungo cha kwenda jela mwaka mmoja na nusu.

Edler na Svensson walikuwa wamehukumiwa na kulipa faini hiyo au kutumikia kifungo hicho baada ya kukiri tuhuma za kuajiri raia wa nje ya nchi na kujihusisha na kazi bila ya kuwa na kibali nchini

Wakati hukumu ikisomwa mahakamani hapo leo Juni 3,mwaka 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo washtakiwa hao raia wa Swiden wanakabiliwa na mashtaka mawili, likiwemo la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali.

Baada ya kusomewa mashtaka yao, washtakiwa wamekiri na wamehukumiwa kulipa faini au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani.

Mapema akisoma mashtaka yao, Wakili wa Serikali Daisy Makakala amedai kati ya Agosti 18 mwaka Jana na Aprili 3, 2019 huko Mikocheni jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Elder akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Biabana Ltd alimuajiri Anders na kufanya kazi katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka idara yavUhamiaji.

Katika shtaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo mshtakiwa Enders alijihusisha na kazi kama muajiriwa wa kampuni ya Biabana LTD bila ya kuwa na kibali kinachotolewa na idaravya Uhamiaji.

Hata hivyo wamefanikiwa kukwepa kifungo cha kwenda ndani jela mwaka mmoja na nusu jela baada ya kulipa faini ya Sh.milioni 20 kwa kila mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...