Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
UBALOZI wa India nchini Tanzania umewahamasisha Watanzania kuendelea kushiriki kufanya mazoezi kwa ajili ya kuweka miwili yao katika hali nzuri kiafya.
Umetoa kauli hiyo leo Juni 23 ,2019 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakati wa Siku ya Kimataifa ya Yoga ambapo mamia ya raia wenye asili ya India waishio nchini pamoja na baadhi ya Watanzania wameshiriki kufanya Yoga.
Kwa kukumbusha tu Yoga ni aina ya michezo yenye kutumia akili na maarifa na lengo kuu ni kuweka miwili katika hali nzuri kiafya ikiwa na pamoja na kukabiliana na kuondoa baadhi ya magonjwa mwilini.Yoga mara nyingi hufanyika kuanzia saa 12 asubuhi.
Akizungumza kabla na baada ya kufanyika kwa Yoga ,Balozi Mdogo wa India nchini Tanzania Rama Chandran Chandramouli amesema mchezo wa Yoga asili yake ni India na leo unafanyika katika nchi mbalimbali Duniani, hivyo Tanzania nayo wameshiriki kwa raia wa India wanaoishi nchini na Watanzania mbalimbali kucheza Yoga.
Amesema kikubwa ni kuhakikisha jamii inajenga utamaduni wa kushiriki mchezo wa Yoga ambao unafaida nyingi kwa anayeushiriki kwani humsaidia kumjenga kimwili na kiakili."Yoga ni mchezo ambao hautaji sehemu kubwa ili uucheze wale gharama.Unaweza kucheza hata ukiwa nyumbani au popote pale.Hivyo nitoe rai kwa wote ambao wameshiriki leo na wengine wote kucheza Yoga,"amesema.
Bolozi Rama Chandrani amesema pamoja na Yoga kufanyika leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa Duniani ya Yoga, bado kila mmoja wetu anayo nafasi ya kufanya Yoga kila anapopata nafasi kwani mbali ya kuweka mwili katika afya njema pia inasaidia kuweka sawa mfumo wa upumuaji kutokana na aina ya staili za mchezo huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Omary Yusufu Single amesema umefika wakati kwa Watanzania kuanza kucheza Yoga kwani ni mchezo mzuri kiafya.
Single ambaye alimuwakilisha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk.Harson Mwakyembe aliyekuwa mgeni rasmi amesema Tanzania kuna michezo michache,hivyo ni wakati sahihi Yoga kupewa nafasi na kwamba watawaweka mkakati kuhakikisha unafahamika kila mahali.
"Tutaweka mkakati utakaowezesha mchezo wa Yoga kuenea maeneo mbalimbali ya nchi yetu.Kwa siku ya leo kuna idadi kubwa ya Watanzania wamejitokeza kushiriki.Pia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari 17 nao wameshiriki Yoga.Kwa upande wetu Serikali tutaendelea kutoa jamaa ili watu wengi zaidi washiriki,"amesema Singo.
Akifafanua zaidi kuhusu Yoga,amesema awali siku hiyo ilikuwa inafanyika maeneo ya Coco Beach jijini Dar es Salaam lakini Dk.Mwakyembe kwa kutambua ukubwa na heshima ya siku hiyo alitangaza Siku ya Kimataifa ya Yoga iwe inafanyika Uwanja wa Taifa,hivyo huu ni mwaka watatu inafanyika hapo.
Baadhi ya wanafunzi ambao wameshiriki katika siku ya Yoga wameiomba Serikali kuangalia namna ya kuupeleka mchezo huo katika shule zote nchini kwani unafanyika katika maeneo salama na faida zake kiafya ni nyingi.
Baadhi ya Washirki wa Yoga wakiendela na mazoezi ya Yoga leo ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Yoga Duniani ambapo kwa Tanzania imefanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Balozi wa India nchini Tanzania Rama Chandran Chandramouli (kushoto) akizungumza kabla ya kuanza kwa Yoga leo katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.Kulia ni mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Omari Yusuf Single
Balozi Mdogo wa India nchini Tanzania Rama Chanran Chandramouli (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakishiriki Yoga leo Juni 23,2019 katika Viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam
Sehemu ya washiriki wa Yoga wakiendelea na mazoezi katika Viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam wakati wa Siku Kimataifa ya Yoga
Baadhi ya washiriki wakiendelea kufanya Yoga kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Washiriki wa Yoga wakiendelea na mazoezi iliyofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam
Mmoja ya waongozaji wa Yoga akifanya mazoezi ya Yoga leo Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo(wa pili kulia mstari wa mbele)Omar Yusufu Single akishiriki kwenye Yoga leo katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam
Washiriki wa Yoga wakiendelea na mazoezi ya Yoga leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Sehemu ya washiriki wa Yoga wakiendelea kufanya mazoezi ya Yoga leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...