Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MESUT Ozil, mshambuliaji wa timu ya Arsenal na aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani amemuoa mchumba wake waliodumu kwa muda mrefu ambaye ni muigizaji, mwanamitindo na aliyekuwa mrembo wa Uturuki (Miss Uturuki) Amine Gulse huko Instanbul katika hoteli ya kifahari iliyo pembezoni mwa mto Bospherous huku Rais wa nchi hiyo Tayyip Erdogan akiwa mpambe na kushuhudia wawili hao wakioana.
Harusi hiyo iliyofanyika siku ya jana ilihudhuriwa na wageni wapatao 300, huku ikielezwa kuwa wanandoa hao walichumbiana mwaka 2017 na kuweka wazi mahusiano yao mwaka 2018.

Mwezi Machi mwaka huu Ozil alitangaza kuwa Rais wa Uturuki atakuwa mpambe wake siku ya harusi yake ambapo alipingwa vikali na wadau wa soka duniani kwa kuhusisha jambo hilo na masuala ya kisiasa.
Ozil mzaliwa wa ujerumani (Gelsenkirchen,) mchezaji wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki aliondoka Ujerumani mwaka jana baada ya kushutumiwa vikali baada ya picha aliyopiga na Rais Erdogua kusambaa ikiwa ni muda mchache kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia 2018 yaliyofanyika nchini Urusi.
Ozil alijitoa kundini na kueleza kuwa amekuwa akichukuliwa kuwa raia wa Ujerumani wanaposhinda na mhamiaji wanapopoteza mchezo.
Mesut Ozil mshambuliaji makini ambaye pia amewahi kukipiga katika klabu ya Real Madrid ameingia katika orodha ya kusimamiwa ndoa yake na Rais Erdogan ambaye pia amewahi kuwa mpambe katika harusi ya aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Newcastle Emre Belozogla.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...