Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Kanda ya Kaskazini imetambulisha rasmi kwa wadau wa mawasiliano mkataba wa huduma kwa wateja ambao ulikwishazinduliwa tayari rasmi Mei 8 mwaka huu.
Akizungumzia na waandishi wa habari wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya mawasiliano kutoka Kanda ya Kaskazini ambacho kimefanyika leo Juni 26,2019 Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA)Mhandisi Imelda Salum amesema lengo ni kubadili mambo mbalimbali yahusiyo taarifa za mawasiliano
Amesema kwamba mkataba huu unakusudia kuongeza uelewa wa wadau kuhusiana na mamlaka ,huduma zinazotolewa na mamlaka,haki na wajibu wa wateja na pia utaelezea jinsi ya kuhamasisha wadau wasioridhika na huduma wanazozitoa
Aidha amebainisha pia mkataba huo utasaidia kuwafanya watumishi kuwa na mtazamo wa kujali na kuheshimu zaidi mahitaji ya wateja pamoja na wadau wote kwa kuwahudumia bila ubaguzi wowote ule
Amefafanua kuwa lengo kuu la kuboresha haya yote likiwa ni kuboresha maisha ya Watanzania kupitia uthibiti wenye ufanisi ambao unachochea na kukuza ubunifu ambao unahakikisha upatikanaji wa huduma bora na imara za mawasiliano ambazo zinatolewa kwa gharama nafuu zaidi.
Amesema mkataba huo utasaidia kujua namna gani ya kuhudumia jamii kwa ujumla na kuboresha sekta ya mawasiliano pamoja na kutatua changamoto zilizopo.
Aidha amewashauri wadau wote wanaotumia huduma zinazotolewa na mamlaka kuhakikisha wanajua vizuri sheria ,kanuni ,miongozo na taratibu za mamlaka ili kuzifuata vyema sheria zinazongoza matumizi ya huduma za mawasiliano
Kikao hicho kimefunguliwa leo jijini Arusha na kimeshirikisha wadau wa mawasiliano kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini ambayo ni Tanga,Arusha Manyara na Kilimanjaro.
Kaimu mkuu wa kanda ya kaskazini mamlaka ya mawasiliano TCRA Mhandisi Imelda Salum akimkabidhi leseni ya kurusha matangazo mkurugenzi wa Radio Kicheko Live ,Phlaviana Kavishe ya mkoani kilimanjaro .
kaimu mkuu wa kanda ya kaskazini mamlaka ya mawasiliano TCRA Mhandisi Imelda Salum akiongea na wadau wa mamlaka ya mawasiliano katika ukumbi wamkutano katika jengo la mkuu wa mkoa wa Arusha
wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...