Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA imeweka mifumo maalum ya udhibiti wa usalama wa chakula kinachozalishwa ndani ya nchi na kile kinachoingizwa kutoka nj e ili kuhakikisha afya bora kwa walaji.

Mifumo hii ni kufanya tathmini ya vyakula vilivyofungashwa,kusajili maeneo na kutoa vibali vya biashara za vyakula, kufanya ukaguzi wa vyakula katika soko pamoja na ukaguzi wa maeneo ya kusindikia, kuhifadhia na kuuzia vyakula.

Akizungumza wakati akifungua Semina ya siku mbili kwa waandishi wa Habari iliyofanyika Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa chakula TFDA Moses Mbambe alisema mifumo hii pia husaidiwa na  uchunguzi wa sampuli za vyakula katika maabara.

“Ndugu zangu Waandishi wa Habari, naomba muufahamishe Umma kuwa mifumo hii inahakikisha kila Mtanzania anatumia chakula salama, na tunaanzia mipakani na kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini” alisema Mbambe.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu Usalama wa TFDA Bw. Adam Fimbo alisema umuhimu wa usalama wa chakula Nchini Tanzania unapewa kipaumbele kwa kushirikiana na Baraza Kuu la umoja wa mataifa ambapo kupitia kikao chake cha Desemba 28 2018 ilipitisha siku ya usalama wa Chakula Duniani kuwa   Juni 7 ya kila mwaka ambapo kwa mara ya kwanza Duniani kote siku hiyo ilianza mwaka huu wa 2019.

“Tanzania tunaungana na Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha tunakuwa na kiwango cha hali ya juu cha usalama wa chakula,tunawaomba wananchi wazingatie uzalishaji bora wa vyakula na hii   itaongeza ufanisi na kuimarisha afya za wananchi wetu” alisema Fimbo

Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani WHO takribani Watu Milioni 600 Duniani sawa na Mtu mmoja kati ya watu 10 huugua kila mwaka kutokana na kula chakula kisicho salama na kati yao watu 420,000 hufariki  na huku watoto wakiwa  125,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano ambapo kwa Bara la Afrika zaidi ya watu milioni 91 wanakadiriwa kuugua huku watu 137,000 hufariki dunia kila mwaka.


Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bw. Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akifungua kikao kazi leo katika ukumbi wa Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.
Kaimu Mkurungezi wa Usalama wa Chakula wa (TFDA),Moses Mbambe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusajili vyakula ili kuhakikisha vinakidhi  viwango vilivyoweka kabla ya kuruhusiwa kwenye soko la Tanzania.
Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) , Bi. Gaudensia Simwanza akizungumza na waandishi wa habari kuhusu usalama wa chakula na kuwawezesha kutoa taarifa sahihi kwa jamii wakati wakiandika habari zihusuzo chakula,kwenye kikao leo katika ukumbi wa Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv Pwani)

Waandishi wa habari  wakiendelea na kikao katika ukumbi wa Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.
Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijirii kwenye kikao hicho leo katika ukumbi wa Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...