Juni 21/2019 timu ya wataalam Saba toka Wizara ya Uchumi na Fedha ya Serikali ya China ilitembelea eneo la ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Leadership School, kilichopo Kibaha kwa Mfipa kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.

Mratibu wa ujenzi huo Bi. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda alieleza kuwa, ukaguzi huo unaotarajia kuchukua siku kumi unafanyika kwa mara ya kwanza ikiwa shughuli zote za ujenzi wa msingi, nguzo na kuta za majengo yote umekamilika. 

Pamoja na mambo mengine wakaguzi hao wanaangalia uimara na ubora wa majengo, kabla ya kutoa kibali kwa mkandarasi kampuni ya CRJE kuendelea na ujenzi. 

Aidha Bi. Kaganda alieleza kuwa ukaguzi wa pili utafanyika katika hatua za mwisho za ujenzi miezi michache ijayo huku wa mwisho ukitarajiwa kufanyika baada ya ujenzi kukamilika na kabla ya mradi kukabidhiwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mradi wa ujenzi wa chuo hicho cha mafunzo ya itikadi na uongozi chenye uwezo wa kufundisha viongozi 200 kwa wakati mmoja, kinachomilikiwa na CCM kwa kushirikiana na vyama vya ANC, Afrika Kusini; ZANU PF, Zimbabwe; FRELIMO , Msumbiji na SWAPO, Namibia, ulizinduliwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania mwezi Julai 2018 na kinatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Juni 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...