Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii
IMEELEZWA  kwamba baada ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini kudhibiti uingizwaji na biashara ya dawa hizo hivi sasa waliokuwa wanajihusisha na utumiaji wa dawa hizo wanahaha kutafuta mbadala wake ili kupata stimu kiasi cha baadhi yao kuanza kuvuta sumu ya panya.

Baadhi ya wamiliki wa nyumba za kuhudumia walioathirika na utumiaji wa dawa za kulevya nchini wameiambia Michuzi Blog kwenye mahojiano maalumu kuwa upatikanaji wa dawa za kulevya kwa sasa umekuwa mgumu, hivyo wanaondelea na utumiaji wa dawa hizo wanahaha katika kuzipata kwake, hivyo wapo ambao wanatumia dawa za hospitali na wengine wanatumia sumu ya panya.

Mmoja wa wamiliki wa nyumba za Sober House kutoka New Vision Society Hamis Shuila amesema kazi nzuri ambayo inafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini, kupitia Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, huko mtaani waliokuwa wanajihusisha na utumiaji wa dawa wapo katika wakati mgumu sana.

"Tunatoa huduma kwa walioathirika na dawa za kulevya na wameamua kuacha kwa hiyari yao.Hata hivyo hata wale ambao wanaendelea kutumia dawa za kulevya wanaishi maisha magumu.Ni ngumu sana kupata dawa ya kulevya kama ilivyokuwa huko nyuma.Ndio maana wengine wanalazimika kutumia dawa za hospitali kama mbadala wa dawa za kulevya.Wanatumia na wanapata stimu kama kawaida.

"Pia wapo ambao wao hawawezi kupata dawa za hospitalini, hivyo wanachokifanya wanachukua hii sumu ya panya ambayo unaijua wewe na kisha kuichanga kwenye kwenye bangi na baada ya hapo wanavuta na hakuna utofauti kati ya sumu ya panya  iliyochanganywa kwenye bangi na dawa za kulevya.Stimu ni ile ile tu na wanalewa vizuri,"amesema Shuila.

Amefafanua wanaotumia sumu ya panya kwa kuchanganya kwenye bangi na kisha kuvuta au kutumia dawa za hospitali si kwamba wanapenda ila kinachotokea watumiaji wa dawa za kulevya ni wagonjwa na hivyo wanatafuta mbinu yoyote kujitibu na hasa kwa kuzingatia akikosa kuvuta mwili unakuwa na maumivu makali sana.

"Hawa wanaotumia dawa za kulevya tunawaita ni wagonjwa na wakati mwingine wanakuwa kama wagonjwa wa akili.Hata hivyo akikosa dawa anakuwa na alosto ambayo hiyo itamfanya atumie mbinu yoyote kupata dawa, hata wale ambao unaona wamepora,wamejeruhi ili kupata fedha wanachotafuta ni kujitibu yale maamivu ambayo wanayasikia, hivyo wako tayari kufanya chochote na hajali hata kufa,"amesema Shuila.

Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa Watanzania kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya kwani madhara yake ni makubw kwa jamii, na kwamba wapo wengi waliokuwa wanatumia dawa hizo na sasa wameacha na kubaki kuwa watu weme na wanaendelea na majukumu yao ya ujenzi wa familia na nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Peter Mfisi amesema kutokana na kuzibwa kwa njia zote za kuingizwa kwa dawa za kulevya kumesababisha watumiaji kutafuta njia mbadala na hivyo wapo
wanaotumia dawa za hospitali kuvuta.

Hata hivyo ametoa ombi kwa watumishi wa  Hospitali, vituo vya afya, maduka ya dawa pamoja na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuhakikisha dawa zilizopo hospitalini zinatumika kwa mujibu wa utaratibu ikiwa pamoja na kutumiwa kwa wagonjwa husika na kwa maelekezo ya daktari na si kuacha zikaingia mtaani na kutumika kama dawa za kulevya.
 Waziri wa  Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Mkuchika (wa tatu kushoto)aliyemuwakilisha mgeni rasmi mama Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo kitaifa imefanyika Tanga akipiga makofi
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Mkuchika aliyemuwakilisha Makamu wa Rais kwenye Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani akiwa katika banda la Uhamiaji akipata maelezo ya namna  wanavyoshiriki kupambana na dawa za kulevya.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wakiwa kwenye maandamano ya Siku ya Kulevya Duniani ambayo kufanyika kila Juni 26 na mwaka huu imefanyika katika Jiji la Tanga
 Baadhi ya waigizaji films nchini kutoka  Bint Filamu wakiwa pamoja na baadhi ya wachezaji mpira kabla ya kuanza kwa maandamano ya kuelekea viwanja vya Tangamano jijini Tanga ambako yamefanyika Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani
 Kiongozi wa Kundi la Wazale ndo Kwanza ambako limejimuisha wasanii mbalimbali  Stive Nyerere akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Mkuchika wakiwa wameshika tuzo iliyotolewa na  Bint Filamu katika kutambua mchango wa Serikali katika mchango wa Serikali katika mapambano ya vita dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Mmojawapo wa waathirika wa dawa za kulevya, Said Bandawa akitoa ushuhuda wa namna Serikali ilivyomsaidia kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya kupiga vita Dawa za Kulevya duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano, jijini Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...