Wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi wao, Bella Bird, wamefanya usafi kwenye fukwe za bahari eneo la Coco Beach jijini Dar Es Salaam.
Usafi huo ulifanyika kama jitahidi za Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira.
“Ujumbe wetu kwa jamii ni wawe na wajibu wa kuepuka uchafuzi, kuondoa utamaduni wa kutupa taka ovyo na kua na tabia ya kuchakata. Tumefurahi Serikali imechukua hatua kubwa kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki na tunatumaini wataendelea kudhibiti",alisema Bird.
Aliendelea kusema kwamba upungauaji wa taka za mifuko ya plastiki hakika ni kitu kikubwa kwa Tanzania kusherehekea. Pia alisema hatua itayofuata ni kupiga marufuku mirija ya vinywaji kwa kua haina matumizi yoyote muhimu kwa karne hii.
Nao wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania walisema kila mmoja ana jukumu la kutunza mazingira.
"Wote tunajukumu kwenye hizi taka. Makampuni ya vyakula na vinywaji yashiriki kutoa elimu kwa jamii, kupanga usafi, kuweka pipa za taka na kusaidia uzoaji taka kama jukumu la kampuni kwa jamii",walisema wafanyakazi hao.
Nae, Carlos Mdemu ambaye ni mratibu wa 'Nipe Fagio' alisema “kuweka pipa za taka maeneo ya fukwe na mtaani ni mpango mzuri, lakini kwenye baadhi ya maeneo tumeona mapipa yanajaa na hakuna anayekuja kuyazoa, kwahiyo watu wanabidi wajue majukumu yao pia”.
Mdemu aliendelea kusema “kuwatoza faini kwa kutupa taka ovyo inafanywa na Manispaa ya Ilala na ni nzuri. Lakini kuongeza ufahamu inaweza kua muhimu zaidi ili kwamba watu wengi wakiwa wanajua, unapunguza nguvu ya kuwatoza faini”.
Kuhusiana na taka za plastiki Mdeme alisema “kwa sasa, taka yenye changamoto tuliyoona ni chupa za plastiki zenye rangi na vifungashio vya chakula (aiskrimu n.k). Chupa za plastiki za rangi hazikusanywi kwa ajili ya kuchakata kwasababu hazina soko kwa wakusanyaji”.
“Hapo nyuma tulipofanya usafi wa fukwe, tuligundua hesabu za taka za mifuko ya plastiki ni zaidi ya asilimia 50. Hii imebadilika, leo tumekusanya si zaidi ya asilimia 10” alisema Carlos Mdemu.
Wakihitimisha usafi katika fukwe za Coco Beach wafanyakazi hao walisema "tumeacha alama ndogo ukilinganisha na kinachotakiwa kufanywa. Lakini hii ndiyo sababu kwanini tumefanya na kwanini wote inabidi tuunganishe mikono na kuacha alama kubwa zaidi.
"Tunatekeleza tunachokisema, Benki ya Dunia Tanzania tunasema hapana kwa plastiki, weka fukwe na bahari yetu safi, sema hapana kwa matumizi ya plastiki, saidia mapambano dhidi uchafuzi wa plastiki" walisema wafanyakazi hao.
Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini, Bella Bird (kushoto) akiwa
amejumuika na baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo baada ya kuhitimisha
zoezi lililofanyika katika eneo la fukwe za bahari ya Coco Beach
walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono
mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo
ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini, Bella Bird (wa pili kulia) akipata
maelezo kutoka kwa Carlos Mdemu (wa tatu kushoto) ambaye ni Mratibu wa
Nipe Fagio baada ya kuhitimisha zoezi hilo lililofanyika katika eneo la
fukwe za bahari ya Coco Beach wafanyakazi hao walipojitolea kusafisha
fukwe hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti
matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha
uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.Pichani walioinama chini ni
vijana wa Nipe Fagio wakijaribu kufanya tathmini ni taka gani zaidi
zimejitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la usafi katika fukwe hizo.
Mratibu
wa Nipe Fagio, Carlos Mdemu na vijana wake wakichambua sehemu ya taka
za plastiki ziliookotwa na wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya
Tanzania walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga
mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo
ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam
huku Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini, Bella Bird na
baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakitafuta ufumbuzi wa kuhakikisha
bahari inakuwa safi na salama kwa viumbe wanaoishi baharini.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania wakiokota taka za
plastiki zikiwemo chupa za vinywaji vya MO Energy vya kampuni ya MeTL na
mifuko ya lambalamba za Ukwaju zinazotengenezwa na kampuni ya Azam
iliyokuwa imetapakaa katika eneo la fukwe za bahari ya Coco Beach
walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono
mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo
ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania wakionyesha taka za
plastiki ikiwemo miraji na mifuko ya lambalamba bidhaa za Ukwaju
zinazotengenezwa na kampuni ya Azam iliyokuwa imetapakaa katika eneo la
fukwe za bahari ya Coco Beach walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa
ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya
mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa
mazingira jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania wakiwa wamebeba
mifuko ya kuhifadhi taka walipokuwa katika eneo la fukwe za bahari ya
Coco Beach walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga
mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki
ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es
Salaam.
Ofisa
Habari wa Benki ya Dunia nchini, Loy Nabeta akionyesha mifuko plastiki
ya lambalamba za kampuni ya Azam iliyokuwa imezagaa katika eneo la fukwe
za bahari ya Coco Beach walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa ni
juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko
ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira
jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania wakirejea na mifuko
iliyosheheni taka za plasitiki baada ya kuhitimisha zoezi hilo eneo la
fukwe za bahari ya Coco Beach walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa
ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya
mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa
mazingira jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania wakiwa katika picha
ya pamoja na mifuko ya kuhifadhia taka baada ya kuhitimisha zoezi
lililofanyika katika eneo la fukwe za bahari ya Coco Beach walipojitolea
kusafisha fukwe hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali
kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo
kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.
Baadi
ya taka za mifuko plastiki ya lambalamba za kampuni ya Azam pamoja na
chupa za vinywaji vya kampuni ya MeTL zilizochambuliwa na vijana wa Nipe
Fagio baada ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania
kumaliza zoezi la usafi katika fukwe za bahari ya Coco Beach ikiwa ni
juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko
ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira
jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...