Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 
Wafanyakazi wa wa serikali wanatakiwa kutumia mitandao ya kijamii vyema ili kujenga taifa Taifa bora lenye uadilifu na sio kutumia mitandao hiyo kwa kuchafua viongozi wao na kuvuruga amani Hayo yamebainishwa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019 Ndugu Mzee Mkongea Ali wakati kihitimisha ziara ya mwenge wa uhuru kwa Halmashauri ya Arusha ambapo jumla ya miradi nane ilikaguliwa katika halmashauri hiyo 
 Aliwataka wafanyakazi wa serikalini kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya badala yake watumie vyema kwa kuelimisha jamii mambo mema yenye maadili na kunufaisha taifa letu . "unakuta mfanyakazi wa serikali anaovywa na kiongozi wake sasa yeye badala abadilike anaanza kumuandikia vijembe kwenye status pamoja na mitandao mingine yakijamii kitu ambacho sio kizuri "alisema Mzee Mkongea. 
 Aidha alisema kuwa miradi yote iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru katika halmashauri ya wilaya ya Arusha imekidhi vigezo vinavyotakiwa ambapo pia ametoa maelekezo na ushauri wa namna bora ya kuboresha miradi hiyo ili ilete tija nzuri zaidi inayokusudiwa. 
 Aliipongeza halmashauri hiyo pamoja na viongozi wake wakiongozwa na mkuu wa Wilaya hiyo ya Arumeru Jerry Muro kwa jinsi wanavyoisimamia miradi hiyo kwa weledi na uamini na aliwasihi waendelee hivyo hivyo . 
 Miradi nane imetembelewa katika halmashauri hii Katika halmashauri hii ambayo ni mradi wa ufugaji nyuki, mradi wa Maji, mradi wa shule, mradi wa maji wa love, ufunguzi wa kiwanda cha mbegu na madawa .
Akiongea mara baada yakupokea mwenge huo mkuu wa wilaya Mhe. Jerry Muro alisema mwenge huo umefungua jumla ya miradi naneambayo imetembelewa ,uwekaji mawe ya msingi, pamoja na kuzindua miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo ina thamani ya shilingi bilioni 15.9. 
 Alisema miradi hiyo ipo katika sekta za maji, elimu, afya, kilimo, ufugaji, uhifadhi mazingira na uwekezaji. Mwenge wa uhuru bado unaendelea na ziara yake katika wilaya ya Arumeru ambapo leo June 9 mwenge umeingia katika halmashauri ya Meru na utaendelea na kazi ya kukagua, kuweka mawe Ya msingi na kuzindua hii ni kutokana na wilaya ya Arumeru kuwa na halmashauri mbili zenye kata 53
Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Charles Mahera akimkabidhi mwenge wa uhuru mkurugenzi wa halmashauri ya Meru Emmanuel Mkongo tayari kabisa kwa kuukimbiza katika halmashauri ya Meru
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akitaja miradi ambayo mwenge wa uhuru utatembelea katika halmashauri Ya meru ambapo amesema jumla miradi nane itatembelewa yenye thamani ya shilingi  7,005,350,943.50
  Kiongozi wa mwenge akipata maelezo kutoka kwa muguzi wa hospital ya Wilaya Patandi jinsi wanavyowapa wakina mama wajawazito elimu 
Chipukizi wa Meru wakisherehesha
 Viajana chipukizi wa halmashauri ya meru wakisherehesha mara baada yakupokea mwenge
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019 Ndugu Mzee Mkongea Ali akimkabidhi  mama mjamzito Monika Gabriel chandarua kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika chumba cha kuhifadhia maiti iliopo Ndani ya hospitali ya Wilaya  patandi  mkoani Arusha. 
Picha Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019 Ndugu Mzee Mkongea Ali akimkabidhi  mama mjamzito chandarua kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika chumba cha kuhifadhia maiti iliopo Ndani ya hospitali ya Wilaya  patandi  mkoani Arusha. Picha na Woinde Shizza wa  Michuzi TV

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...