Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MKURUGENZI wa kampuni ya Biabana, Anna Kristina Edler, (54) na mumewake, Anders Svensson 58 wamehukumiwa kulipa faini ya sh. Milioni 20 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani baada ya kukiri tuhuma za kuajiri raia wa nje ya nchi na kujihusisha na kazi bila ya kuwa na kibali nchini
Hukumu hiyo imesomwa, leo Juni 3, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo washtakiwa hao raia wa Swideni wanakabiliwa na mashtaka mawili, likiwemo La kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali.
Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka yao, washtakiwa wamekili na wamehukumiwa kulipa faini ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu gerezani.
Mapema akisoma mashtaka yao, wakili wa serikali, Daisy Makakala amedai kati ya Agosti 18 mwaka Jana na Aprili 3, 2019 huko Mikocheni, mshtakiwa Elder, akiwa kama mkurugenzi wa kampuni ya Biabana Ltd alimuajiri Anders na kufanya kazi katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka idara yavUhamiaji.
Katika shtaka la pili imedaiwa, aiku na mahali hapo mshtakiwa Enders alijihusisha na kazi kama muajiriwa wa kampuni ya Biabana LTD bila ya kuwa na kibali kinachotolewa na idaravya Uhamiaji.
Mpaka tunaondoka Mahakamani hapo, wazungu hao walikuwa hawajafanikiwa kulipa fine na wameenda gerezani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...