Na Amisa Mussa
JESHI LA POLISI MKOANI TABORA KWA KUSHIRIKIANA NA KAMATI MAALUMU KUTOKA MIKOA YA SHINYANGA NA TABORA AMBAYO IMEHUSISHA VYOMBO MBALIMBALI VYA ULINZI NA USALAMA IKIWEMO BODI YA SUKARI ,WATAALAMU KUTOKA KIWANDA CHA SUKARI KILOMBERO PAMOJA NA WATAALAMU WENGINE KUTOKA TAASISI ZA TFDA, TRA, WAKALA WA VIPIMO NA OFISI YA MKURUGENZI WAMEENDESHA OPERATION MAALUMU YA KUKAGUA BIDHAA MBALIMBALI ZA CHAKULA HUKO MKOANI TABORA NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WAFANYABIASHARA WATANO WAKIWA NA VIFUNGASHIO MBALIMBALI VYA BIDHAA AMBAVYO SI HALISI (FAKE) .
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Tabora Kamishna Msaidizi Wa Jeshi La Polisi EMMANUEL NLEY Anasema Wafanyabiashara Hao Watano Ambao Kwa Sasa Wote Wapo Mikononi Mwa Jeshi La Polisi Mkoani Humo Wamekua Wakibadilisha Kwenye Vifungashio Sukari Ya Kiwanda Cha Kutoka Nje Ya Nchi Na Kuiweka Kwenye Mifuko Ya Kiwanda Cha Kilombero Ili Waweze Kuuza Kwa Bie Ya Juu Huku Wakipunguza Ujazo Wa Mafuta Kwenye Bidhaa Ya Mafuta Ya Korie Lita Moja Kwa Kila Lita Ishirini Wakitafuta Faida
Wakati Huohuo KAMANDA NLEY Amesema Watu Wanne Wanashikiliwa Na Jeshi La Polisi Wakiwemo Watumishi Wawili Wa Bohari Ya Dawa Mkoa Wa Tabora Msd Kwa Tuhuma Za Kuiba Dawa Aina Ya ALU Maarufu Dawa Mseto Wakidaiwa Walikua Wakisafirisha Kupeleka Nchi Jirani
Aidha KAMANDA NLEY Amebainisha Kuwa Watuhumiwa Wote Ambao Kwa Sasa Wapo Mikononi Mwa Polisi Watafikishwa Mahakamani Mara Baada Ya Upelelezi Kukamilika.
SEHEMU YA SHEHENA YA DAWA ALMAARUFU KAMA DAWA MSETO
KAMANDA WA POLISI MKOA TABORA ACP EMMANUEL NLEY
VIFUNGASHIO MBALIMBALI VYA BIDHAA AMBAVYO SI HALISI(FAKE)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...