NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

SERIKALI mkoani Pwani ,imewaasa wenye viwanda kuhakikisha wanazalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya kisheria ya vipimo, ili kumlinda mteja,uchumi wa nchi na kupata tozo stahiki.

Aidha ,mamlaka za maji na jamii zimetakiwa kupeleka mita za maji kupima kwa wakala wa vipimo ili kuondoa malalamiko mbalimbali ikiwemo ubovu wa mita ama matumizi ya maji yasiyoendana na malipo .

Akitoa rai hiyo ,wakati alipotembelea mitambo ya kituo cha upimaji wa vipimo huko Misugusugu ,Kibaha,mkuu wa mkoa huo, Mhandisi Evarist Ndikilo alieleza,yapo malalamiko kutoka kwa baadhi ya viwanda wakiona wanabughudhiwa lakini ni lazima wazalishe bidhaa zinazoendana na vipimo.

“Viwanda vya saruji vizalishe saruji inayoendana na uzito sahihi na vipimo sahihi,nondo, na bidhaa zote zinazozalishwa viwandani ,kuliko kuwa na viwanda vingi vyenye bidhaa zisizo na viwango”alisisitiza Ndikilo.

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa ,alisema mita za maji zimekuwa kero kwa watu wakidai wanaibiwa kuwa haziingiliani na vipimo.“Mamlaka za maji na wananchi walio na kero hizo nendeni kwa wakala wa vipimo ili kuondoa kero hizo”alifafanua Ndikilo.

Awali ofisa mtendaji mkuu wa wakala wa vipimo ,dkt Ludovick Manege alisema kituo hicho kinalenga kupima vimimina vya petrol,dizel na mita za maji.Manege alibainisha kwamba, kwasasa wameunda kikosi maalum kwenda kukagua bidhaa viwandani kuangalia kama zinakidhi matakwa ya kisheria ya vipimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...