Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MRATIBU wa Mradi wa kutoa elimu kuhusu muhimu wa kutumia nishati mbadala Euphrasia Shayo kutoka FORUMCC amesema wanatarajia kutoa elimu hiyo kwa Watanzania milioni tano ndani ya miezi 20 kuanzia Mei mwaka huu.
Shayo amesema hayo wakati wa maadhimisho ya mazingira ambayo kwa Dar es Salaam yamefanyika Viwanja vya Jakaya Kikwete ambapo wadau mbalimbali wa nishati mbadala wameonesha namna ambavyo wanatengeneza bidhaa ambazo lengo lake ni kuhakikisha Watanzania wanakuwa na uelewa wa kutunza mazingira kwa kutumia nishati mbadala.
Akifafanua zaidi Shayo amesema mradi huo unafanyika chini ya ufadhili wa Hivos ambao wako nchini Finland na kwa kutambua muhimu wa kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi wameona haja ya kuufadhili mradi huo wakiamini ni mradi wenye tija kwa jamii.
"Ni mradi ambao FORUMCC tunautekeleza kwa ufadhili wa Hivos ,lengo letu ni kuwafikia Watanzania milioni tano ambao watakuwa na uelewa wa umuhimu wa kutumia nishati mbadala ili kutunza mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,"
Amesisitiza wanatoa elimu ya nishat mbadaa kama njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kuwa na mazingira endelevu na kwamba mradi huo unawalenga wananchi,Serikali, taasisi za umma na binafsi, taasisi za elimu ya juu na vyombo vya habari ambavyo vinamchango mkubwa wa kufikisha taarifa za mabadiliko ya tabianchi na athari zake.
"Kama ambavyo nimeeleza hapo awali,elimu ambayo tunaitoa ni kwa kutumia njia mbalimbali kama kuendesha mauzo kwa kutumia semina,mijadala,kufanya tafiti pamoja na kufuatilia bajeti ya Wizara ya nishati na wizara zinazohusika na mazingira iwapo wanatalenga fedha kwa ajili ya kuhamasisha jamii kutumia nishati mbadala kama njia ya kutunza mazingira.Faida kubwa kwa Hivos ni kuna dunia inakuwa mahali salama kimazingira,"amesema.
Amefafanua kuwa kabla ya kuanza kwa Bunge wadau wanakutana kwa ajili ya kuangalia bajeti kama imezingatia masuala ya mazingira na kisha kama kuna haja ya kutoa mapendekezo basi wanafanya hivyo kwa kuhakikisha wanafuata utaratibu unaohitajika kwani FORUMCC wanashirikiana kwa karibu na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali.
Baadhi ya wadau wa mazingira ambao wameshiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya mazingira ambayo FORUMCC wameshirikiana na Manispaa ya Ilala kuifanikisha, wamesema ni vema jamii ikajikita kutumia nishati mbadala kama njia sahihi ya kutunza mazingira.
Ofisa mauzo wa Kampuni ya Mobisol ambao wanauza Sola Wilson Mosses amesema kuna kila sababu ya wananchi kutumia nishati mbadala kama sehemu ya kutunza mazingira huku akifafanua kwa kutumia umeme wa Sola inasaidia kupunguza hewa ukaa ambayo itasababisha kuchafua mazingira."Umeme wa Sola ni marafiki wa mazingira tofauti na kutumia mafuta kusabisha umeme kwani mafuta yanachafua mazingira,".
Amesema kwa sasa kunamuamko kwa watanzania kwani wengi wao wameona kutumia nishati mbadala kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kila na maonesho ya wiki ya mazingira yaliyoandaliwa na FORUMCC yameongeza chachu ya kutumia nishati mbadala nchini Tanzania.
Baadhi ya akina mama wakiwa wameshika karatasi zenye ujumbe wa kuhamasisha jamii kutumia nishati mbadala ili kinda mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.Kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya Mobisol Wilson Mosses.
Msemaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Tabu Shaibu(wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Rebecca Muna wakipata maelezo kuhusu namna ambavyo nishati mbadala inavyosaidia kutunza mazingira
Mratibu wa Mradi wa kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutumia nishati mbadala unaofadhiliwa na Hivos Euphrasia Shayo (kushoto)kutoka FORUMCC akiwa ameshika karatasi yenya ujumbe unaozungumzia nishati mbadala wakati wa maadhimisho ya wiki ya mazingira .Kulia ni Meneja mauzo wa Kampuni ya Mobisol Wilson Mosses ambao wanauza Sola kama nishati mbadala
Mratibu wa Mradi wa kutoa elimu kuhusu nishati mbadala Euphrasia Shayo kutoka FORUMCC akisaini kitabu baada ya kufika kwenye banda la kampuni ya Mobisol wanaojihusisha na uuzaji wa Sola kama nishati mbadala .Aliyesimama ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo Wilson Mosses
Mariam Tindwa akifafanua jambo kwenye maonesho ya wiki ya mazingira namna ambavyo wanatumia taka kutengeneza nishati mbadala ikiwemo mkaa unaotoka na taka







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...