Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk. Omary Sukari akitoa matone ya Vitamini A kwa mtoto 
Watumishi wa halmashauri wakitumia usafiri wa pikipiki katika kufuatilia zoezi la chanjo linavyoendelea katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma

Baadhi ya watoto waliofika kupata chanjo katika zahanati ya kijiji cha Kikonko katika halmashauri ya Mpimbwe 
Baadhi ya kinamama na watoto wao wakisubiri chanjo katika zahanati ya Kikonko 
********************* 

21.06.2019 

Na Mwandishi wetu, Katavi 

Jumla ya watoto 7,935 wa Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi watarajiwa kupata matone ya Vitamini A na dawa za minyoo katika zoezi la utoaji chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano linatalotarajiwa kukamilika juni 30 mwaka huu 

Akizungumzia zoezi hilo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mpimbwe dk. Sebastian Siwale amesema zoezi hilo litahusisha vituo 15 vya kutolea huduma za afya katika halmashauri hiyo 

Aidha ameongeza kuwa wanakabiliwa na changamoto ya uchache wa vyombo vya usafiri hali inayopelekea wakati mwingine kushindwa kufuatilia kwa karibu jinsi zoezi hilo linavyoendelea katika vituo mbalimbali 

“Tuna gari moja kwahiyo inapotokea kuna mgonjwa inabidi atumie gari hilo kupelekwa hospitali na ufuatiliaji unaahirishwa mpaka gari litakaporejea” alisema dk. Siwale 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi dk. Omary Sukari ambaye alikuwa ameambatana na kamati ya usimamizi wa huduma za afya mkoa wameshiriki katika zoezi hilo ambapo amesisitiza umuhimu wa watoto kupata chanjo 

Dk Sukari amesema matone ya Vitamin A yanasaidia kinga ya mwili wa mtoto dhidi ya maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumwezesha mtoto kuona vizuri .Pia ametoa wito kwa wazazi waliowafikisha watoto wao kupata chanjo kuwa mabalozi wazuri kwa majirani zao ili watoto waote wapate chanjo hiyo 

Nao baadhi ya kinamama waliokutwa katika vituo vya kutolea huduma ya afya wameeleza umuhimu wa chanjo hiyo ikiwa ni pamoja na kumpa mtoto kutibu minyoo inayoshambulia katika tumbo la mtoto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...