SERIKALI imewataka wafanyabiashara kuwasilisha kero zao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi badala ya kubaki wakinung’unika kwani hazitatatuliwa na lengo ni kuwawezesha kufanya biashara zao kwa uhuru ili waweze kulipa kodi.
Kauli hiyo imetolewa Juni 20 na mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro,kwenye kikao cha pamoja cha siku moja cha wafanyabiashara,mamlaka ya mapato,halmashauri ya jiji pamoja na taasisi zingine za serikali wilayani Arusha kilichofanyika ukumbi wa Katibu tawala mkoa kwa ajili ya kusikiliza kero zao.
Daqarrop,amesema wapo baadhi ya wafanyabiashara wana kero zao lakini hawako tayari kuziwasilisha TRA kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi badala yake wamekuwa wakinung’unika hivyo wahakikishe wanaziwasilisha TRA ili waweze kukaa pamoja na kuzipatia ufumbuzi.
Kuhusu maegesho yasiyo sahihi(wrongparking)mkuu wa wilaya,amesema utaratibu wa kufunga cheni kwenye magari yaliyoegeshwa unaofanywa na Longparking, ni uhuni huwa wanavizia magari na kuyafunga cheni kwa lengo la kujipatia rushwa baada ya majadiliano na mwenyegari na fedha wanazolipwa huwa hazipelekwi kunakotakiwa.
Ameiagiza wakala wa bara bara Vijijini Tarura, kuiondoa wakala wa Long parking ,kuanzia Juni 21 eneo hilo kwa kuwa imekuwa ni kero na vikwazo kwa wafanyabiashara na wateja wao akawashauri wenye magari wakiombwa fedha wasitoe bali wampigie simu kwani ni wasumbufu wanalazimisha rushwa .
Kikao kimeagiza magari yaegeshwe kwenye eneo hilo kuanzia makutano ya bara bara ya Masijid Kubha na mpaka Miami beachi hotel na yalipe ushuru wa kawaida ili halmashauri ipate mapato yake kupitia kwa wakal wake.
Kwa upande wao wamiliki wa maduka ya rejareja jijini Arusha wameiomba serikali kuwatafutia Machinga maeneo ya kufanyia shughuli zao kutokana na kodi wanazolipa wakati Machinga hawalipi hivyo wanashindwa kufanya biashara .
Kwenye kikao hicho cha pamoja na wamiliki wa maduka wamesema kuwa wenye maduka wanalipa kodi mbalimbali lakini mbele ya maduka yao Machinga nao wanaweka bidhaa zao hivyo wakaiomba serikali kuwatafutia maeneo mengine .
Mwenyekiti wa wafanyabiashara stand ndogo Joan Minja, pia wamelalamikia Wakala wa maegesho ya magari maarufu (wrongparking) kuwa ni kero wanawakosesha wateja wanaoenda kununua bidhaa kwenye maduka yao.
Minja,amesema utaratibu unaotumiwa na maegesho yasiyo sahihi ni kuwatoza faini ya shilingi 50,000 watu wanaoegesha magari hayo na kuingia ndani ya stand hiyo kwa kisingizio cha maegesho hayo kero na usumbufu unazosababisha kukosa wateja.
Mamlaka ya mapato TRA,mkoa wa Arusha ,imesema itafanyakazi hata siku za mapumziko na siku kuu wakati wa kupokea retun za VAT kutoka kwa wafanyabiashara.
Meneja wa TRA Faustini Mdesa, ameyasema hayo alipokuwa akitolea ufafanuzi hoja za wafanyabiashara ikiwemo kulalama kurejesha retun za VAT siku ambazo sio za kazi lengo ni kuwahudumia walipa kodi.
Akawaonya wafanyabiashara kutokufanya udanganyifu kwenye taarifa za biashara zao kwa kufanya hivyo ni kuikosesha mapato serikali hivyo ambao watagundulika kuwasilisha taarifa zisizo sahihi TRA itawarejea kufanya upya ukaguzi wa hesabu .
Amesema kuwa lengo la TRA ni kuwakuza wafanyabiashara na sio kuwadidimiza hivyo wafanyabiashara wenye malimbikizo ya madeni waende TRA ili kutafuta ufumbuzi wa kulipa madeni yao.
Mdesa,ameema TRA inatoa motisha kwa mwananchi yeyote atakaewezesha kutoa taarifa za kukamatwa kwa wakwepa kodi ,ambapo motisha hiyo itatoa asilimia 3% ya bidhaa itakayokamatwa na kuuzwa kutokana na ukwepaji kodi au shilingi milioni 20 .
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wilaya ya Arusha Adolf Lokeni ,amesema mkutano wa rais Magufuli na wafanyabiashara hivi karibuni uliofanyika Ikulu, umezaa matunda na akawasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi.
Amesema ni kweli wapo baadhi ya wafanyabiasha wana malimbikizo ya kodi na wengine hali zao za kibiashara ni mbaya hivyo akaiomba mamlaka ya mapato TRA mkoa wa Arusha kukaa nao ili wajenge mazingira rafiki yatakayowezesha kulipwa kodi na malimbikizo yaliyopo.
Aidha ,Lokeni, ameitaka halmashauri ya jiji kutokuwafungia wafanyabiashara kuna maduka 50 yamefungwa wiki iliyopita stand ndogo kwa sababu wanadaiwa na akasema rais akishatoa maelekezo hakutoa kwa TRA pekee bali na mamlaka zingine zikiwemo halmashauri kutokufunga biashara.
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...