Baadhi ya watumishi wakihamisha matofali kwenda katika jengo la wazazi linaloendelea kujengwa

Katikati Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Omary Sukari akinyanyua tofali kwa ajili ya ujenzi unaoendelea wa hospitali ya wilaya ya Tanganyika, kulia kwake ni Afisa Utumishi Mkoa wa katavi Bi. Cresensia Joseph

Baadhi ya watumishi wakifanya usafi kwa kufyeka nyasi katika eneo la hospitali ya wilaya ya Tanganyika

Jengo la maabara likiwa tayari limekwishaezekwa
Na Mwandishi Wetu Katavi
Katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma watumishi wa sekretariati ya mkoa wa katavi wamejumuika na mafundi katika kusaidia kazi mbalimbali za ujenzi katika hospitali ya wilaya ya Tanganyika lengo likiwa ni pamoja na kutoa hamasa kwa jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Afisa Utumishi wa Mkoa Bi. Cresensia Joseph amesema lengo la zoezi hilo ni kuunga mkono juhudi za serikali kutoa huduma kwa wananchi
Amesema watumishi wanatambua azma ya serikali ya kufikisha huduma karibu na jamii hivyo nao wamejitoa kwa nguvu zao kushiriki katika ujenzi huo .Aidha baadhi ya watumishi walioshiriki katika zoezi hilo wamesema wanafanya hivyo katika kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kusogeza huduma za afya kwa jamii
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Dkt. Selemani Mtenjela amesema hospitali hiyo ikikamilika itahudumia zaidi wakazi laki tatu wa wilaya hiyo
Ameongeza kuwa hospitali hiyo ikikamilika itawaondolea adha ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 130 wakazi wa wilaya hiyo kufuata huduma za afya katika hospitali ya manispaa ya Mpanda
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...