Na John Woinde Shizza, Arusha

WAZIRI wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuzindua mbio za kimataifa za riadha za John Stephen Akwari zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 9 mwaka huu mkoano hapa.

Akizungumza leo mkoani Arusha Mkurugenzi Mtendaji wa mbio hizo,Sylvestar Orao amesema maandalizi yote ya mbio hizo yamekamilika na kutoa mwito kwa wadau wa mchezo huo kutoka ndani na nje ya nchi kujitokeza kushiriki.

Amesema mbio zenye kauli mbiu "Sisi wote ni wakimbiaji,maisha ni mbio" yameandaliwa mahususi kwa ajili ya kumuenzi mwanariadha wa kwanzakabisa kupeperusha vema bendera ya Tanzania kimataifa mzee Jahn Stephen Akwari.

"Katika mbio hizo kutakuwa na mbio za kilomita 21,kilometa tano na kilometa mbili kwa watoto na kwamba vituo vya kujiandikisha vipo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheik Amri Abeid Karume wa mjini hapa na kingine kipo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam," amesema Orao.

Kwa upande wake Mshauri wa kiufundi wa mbio hizo John Bayo amewataka watu kujitokeza kwa wingi katika mbio hizo kwani michezo hudumisha

amani upendo na umoja na kwamba michezo ni mazoezi ambayo humwepusha mtu na magonjwa mbalimbali.Bayo ameongeza katika mbio hizo mshindi wa kwanza hadi kwa 10 kwa mbio zote watapatiwa zawadi na medali mbalimbali kulingana na aina ya mbio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...