Na Khadija Seif, Michuzi TV
BENKI ya lawapatia wanafunzi suluhisho la migogoro ya kutolipa ada kwa wakati mshuleni.
Akizungumza na Michuzi TV kwenye Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara viwanjwa vya Mwalimu Nyerere kwenye banda lao meneja mahusiano wa Benki ya Amana amesema wanafunzi wengi wamekua wakikumbwa na kadhia ya kurudishwa majumbani kutokana na kukosa ada ya kuwawezesha kuendelea na masomo.
"Benki ya Amana inatoa huduma mpya kabisa ikiwa ni fursa kupata mkopo utakaomwezesha mzazi kumlipia ada mwanafunzi na kuendelea kulipa kidogokidogo kwa muda wa miezi 12,"
Aidha ametoa wito kwa wazazi ambao wangependa kupata fursa hiyo ya mikopo kufika katika Banda lao ili kuwawezesha wanafunzi kuanzia shule ya awali, sekondari pamoja na vyuo kupata uhakika wa elimu na kuendelea na masomo yao bila kukosa vipindi.
"Mikopo hiyo haina liba kutokana na kufata utaratibu,sheria na misingi ya dini ya kiislam,"
Pia ameeleza mbali na kupata fursa hiyo ya mikopo benki hiyo pia inatoa fursa kwa wananchi kujiunga na huduma za kibenki katika msimu hii ya Maonyesho
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...