
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
"UISHI KWA MUDA MREFU MFALME", ni maneno yanayoanza katika wimbo mpya wa mwanadada Beyonce Knowles unaojulikana kwa jina la 'Spirit '
Uingizwaji wa maneno hayo ya Kiswahili katika wimbo huo yamezidi kuiweka lugha ya kiswahili katika nafasi bora zaidi kwa kuwa lugha inazungumzwa kwa kiasi kikubwa duniani (kati ya lugha 10 zinazozungumzwa duniani) na huzungumzwa zaidi nchini Tanzania.
Katika shairi la wimbo Beyonce ameanza kwa kuimba kwa sauti ya juu huku sauti nzito ikirudia maneno ya Uishi kwa muda mrefu mfalme akimaanisha long live the king na kufuatiwa na maneno ya kiingereza ya Rise up to the light in the sky, yeah.... Watch the light lift your heart up na kuendelea.
Wimbo huo umeachiwa Leo Julai 11 na ni wimbo ambao umetumika katika filamu mpya ya Lion King iliyotengenezwa na kampuni ya Disney ya nchini Marekani.
Katika wimbo huo mfalme aliyeimbwa ni simba dume anayepambana kuwa mfalme wa nyika.
Albam hiyo ya Spirit inatarajiwa kuzinduliwa rasmi ndani ya siku tisa zijazo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...