Kufuatia miezi kadhaa ya utafiti makini Selcom Tanzania, kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya huduma za kifedha, imezindua rasmi huduma ya Qwikserv. Huduma hii ya kibenki ya uwakala- shirikishi imeundwa kwa lengo la upatikanaji wa haraka na urahisi wa huduma muhimu za kibenki zikiwemo kuweka na kutoa fedha, kuuliza salio na taarifa fupi, kuhamisha fedha na kufungua akaunti.

 Kutokana na msisitizo wa hivi karibuni kuhusu mfumo wa ushirikishwaji wa masuala ya fedha Tanzania, Qwikserve inalenga kuwafikia watanzania wengi wanaokosa huduma za kibenki ipasavyo.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Selcom, Sameer Hirji amesema, “Misingi yetu inayotuongoza siku zote imekuwa ni kuinua ushiriki katika masuala ya kifedha. Kama watoaji wa huduma, tunaendelea kubuni bidhaa na huduma ambazo zitasaidia ukuaji wa wabia wetu wa taasisi za kifedha.

Kwa kuzingatia hili, Qwikserv imebuniwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha bila gharama kubwa za uwekezaji katika maeneo ambayo hayajitoshelezi. Sambamba na hayo, muundo wetu shirikishi kupitia zaidi ya mawakala 18,000 wa Selcom nchi nzima, unawaruhusu kutoa huduma kirahisi na kuwawezesha kutumia mitaji yao kujiongezea kipato katika mzunguko wa mauzo”.

Selcom imefanikiwa katika utekelezaji wa huduma ya Qwikservkwa NMB Bank, CRDB Bank, NBC Bank, TPB Bank, Amana Bank, Access Bank na Letshego Bank pamoja na benki sita zaidi zilizopo katika uzinduzi wa awali kwenye hatua za majaribio na makubaliano.Selcom ina malengo ya kuingia ubia nabenki zaidi ya 35.

Kutokana na changamoto ya mawakala kutakiwa kujiunga na tasisi za kifedha mbalimbali ili kutoa huduma husika, kupitia Qwikserv, mawakala wataweza kutoa huduma za benki shiriki bila kujiunga na taasisi moja moja kwa kutimia mtaji (float) mmoja. 

Mawakala wengi wamevutiwa kujiunga kutoa huduma za kibenki (Qwikserv) kutokana kulipwa faida nono katika miamala ya kibenki pamoja pamoja na huduma nyengine za Selcom wanazotoa. Mbali na hayo, Selcom iko mbioni kuzindua kuwawezesha mawakala kufanya miamal zaidi ya kiasi cha salio (float) kwenye mashine zao za POS.

Pia Qwikserv inawawezesha wateja kufanya miamala moja kwa moja kupitia simu zao za mikononi. Zaidi ya hayo, wateja wanaweza kuweka pesa taslimu na kuzitoa kupitia kadi zao za benki., Selcom inakiu ya kuona ni jinsi gani benki nyiengine zenye ubunifu zitaisukuma kwa haraka ajenda ya mfumo wa ushirikishwaji wa kifedha Tanzania na kuimarisha jinsi Qwikserv inavyotoa huduma zake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...