TAARIFA ambazo zimetufikia chumba chetu cha habari cha Michuzi Media Group, inaelezea wafanyakazi wa Azam Media wamepata ajali ya gari mkoani Singida leo Julai 8 mwaka 2019.
Kwa Mujibu wa taarifa za awali zinadai kuwa katika ajali hiyo kuna waliopoteza maisha na wengine kujeruhiwa.Walikuwa wanakwenda Chato kikazi kwa ajili ya kuonesha LIVE moja ya matukio ya Rais Dkt.John Magufuli.
Baadhi ya Waandishi waandamizi wa Azam Media wameiambia Michuzi Blog na Michuzi TV kuwa kwa sasa wanasubiri taarifa rasmi kutoka wenye mamlaka ili kuuhabarisha umma na wanaodhaniwa kupoteza maisha na wafanyakazi wingine wakiwamo waandishi na Wapiga picha pamoja na mafundi mitambo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...