Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua Waamuzi Waanne na Makamishna Wawili kutoka Tanzania kusimamia mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

Mwamuzi Hery Sasii atasimama katikati kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Aigle Noir ya Burundi na Gor Mahia ya Kenya utakaochezwa Uwanja wa Prince Louis Rwagasore,Burundi Agosti 11,2019.

Sasii atasaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Frank Komba,Mwamuzi msaidizi namba 2 Ferdinand Chacha,Mwamuzi wa Akiba Emmanuel Mwandembwa na Kamishna wa mchezo anatokea Rwanda,Gaspard Kayijuka.

Aidha Mtanzania Ahmed Mgoyi atakua Kamishna wa mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Gor Mahia dhidi ya Aigle Noir utakaochezwa kati ya Agosti 23,24 na 25 nchini Kenya.

Naye Mtanzania Khalid Abdallah ameteuliwa kuwa Kamishna wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Proline FC ya Uganda na Master Security Services ya Malawi utakaochezwa Uwanja wa Kampala Startimes nchini Uganda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...