Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja ametembelea mradi wa kupeleka Majisafi na salama katika mji wa Chalinze wenye thamani ya Bilioni 16 unaotarajiwa kumalizika mwezi Aprili 2020. Amewahakikishia wakazi wa Chalinze tatizo la Maji katika mji wao kubaki kuwa historia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja ametembelea mradi wa maji wa Chalinze Mboga utakaomalika mwezi April 2020.
Mradi huo wa kimkakati wa kupeleka majisafi na salama katika mji wa Chalinze hadi kiwanda cha kusindika matunda cha sayona unaojengwa na DAWASA kwa thamani ya Shilingi Bilioni 16.
Luhemeja ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na mkandarasi ambapo kwa sasa ulazaji wa mabomba ya kusafirishia maji yameshalazwa.
Aidha, Luhemeja amewakikishia wakazi wa chalinze kwamba mradi huo utamalizika mwezi april mwaka ujao na kufanya tatizo la maji katika mji wa Chalinze kubaki kuwa historia.Kukamilika kwa mradi huo kutahudumia maeneo ya Ruvu darajani, Vigwaza,Ranchi ya Taifa Ruvu (NARCO), Chahua -Lukenge, Visenzi, Buyuni na Mdaula -Unebazomozi.
Kwingine ni Chamakweza, Pingi, Pera, Chalinze, Chalinze Mzee, Msoga na Mboga aidha, viwanda vitakavyofaidika ni pamoja na Twyford, kiwanda cha ngozi, kiwanda cha Matunda cha Sayona pamoja na watumiaji wengine wakubwa ikiwemo kampuni Yapi Merkezi wajenzi reli ya kisasa (SGR)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...