Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha 

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha wameitikia Wito wa kuhudhuria Kikao cha ndani kilichoandaliwa na Wazee wa Mila ya Kimasai kwa kushirikiana Mahususi Kwa Kusikiliza Mgogoro uliopo Kati ya Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Manongi na Wananchi wanaoishi Katika Hifadhi hiyo. 

Wazee hao wakiwakilisha Makundi mbalimbali ya Wafugaji, Wanawake, Watumishi walioachishwa Kazi Katika Hifadhi hiyo walilalamikia Kwa vilio na Masikitiko Makubwa Kutokana na Unyanyasi Mkubwa Kutoka Kwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Manongi.

Wananchi hao walilalamikia mbalimbali yakiwemo Kuharasiwa Kila kukicha na askari usu wa Hifadhi hiyo ya Ngorongoro tofauti na ilivyokuwa huko nyuma miaka zaidi ya Kumi iliyopita pia walisema jambo lingine linalowakera ni pamoja na Ardhi yao Kuendelea kumegwa na Hifadhi ya Ngorongoro ambapo walisema hawashirikishwi Katika Matumizi mbalimbali ya Ardhi Katika Maeneo wanayoishi.

Aidha walilalamikia kitendo Kunyimwa Kujiletea Maendeleo na huduma Muhimu Kwa Kujenga Shule, Kanisa na Zahanati huku wakibainisha kuwa walijitoa Kwa nguvu zao ili Kujenga Shule Kwa ajili ya watoto wao lakini badala yake juhudi hizo zimezuiliwa na kuwekwa katazo kabisa la kutojengwa shule, zahanati, Kanisa na hata Majengo ya nyumba za asili Au Kudumu za kuishi.

"Katika Maeneo tunayoishi wananchi tuna Changamoto ya Usafiri hivyo hulazimika Kutumia Usafiri wa Pikipiki (bodaboda) ili kufikia huduma muhimu za afya pindi akina Mama wajawazito na wagonjwa wanakwenda kutafuta huduma ,sisi Wananchi tumezuiliwa Matumizi ya Bodaboda ,Pikipiki na magari binafsi na Mwananchi yeyote atakayeonekana anatumia Pikipiki anakamatwa na kupigwa, kuwekwa ndani na Kunyanganywa Pikipiki yake ,Ikumbukwe Mwaka 2017 ulitokea mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu ambapo Usafiri wa Pikipiki ulitumika kuokoa Maisha ya ndugu zao"alisema mengori laizer

Aidha Wakinamama walilalamikia kuzuiwa kuchota maji Katika mto unaopita Katika Maeneo wanaoishi Kwa ajili ya Matumizi Kibinadamu na kunyweshea mifugo yao. 

Walisema kuwa Menejimenti ya Hifadhi ya Ngorongoro imeshidwa Kushindwa kuiongoza na kuisimamia vizuri Hifadhi hiyo kwani Ndugu Manongi ametafutwa na kuombwa mara nyingi mno ili kukaa pamoja Kwa ajili kutatua changamoto mbalimbali na kuweka namna nzuri ya Mambo kadha wa Kadha lakini Wananchi hao wamesema Rais Magufuli anapatikana wakati wote na Ndugu Manongi yuko busy siku zote. 

Wananchi hao wamewaomba viongozi hao wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha waliofika Kusikiliza kero zao kuzifikisha kwa Rais Magufuli ambaye wamesema pamoja na upepo wa Uchaguzi wa Mwaka 2015 lakini Ngorongoro waliendelea kuwa waaminifu kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi akiwemo yeye Rais Magufuli, Mbunge wao na hakukuwa na Kata hata moja iliyobebwa na Wapinzani na Kwamba wanamfahamu vizuri Rais Magufuli ni Rais wa Wanyonge hivyo wameomba sasa Serikali itamke kitu juu ya Changamoto zao ambazo kiukweli imekuwa ni tatizo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Comrade Loata Sanare alisema kuwa wamesikia changamoto zao na waliwahaidi kuzifanyia kazi kero hizo zote na changamoto zote ambazo zinawakabili.

"napenda kuwahaidi kuwa changamoto zenu zote tumezikia na sisi kama viongozi wa ccm chama ambacho kinashika dola tunawahaidi kuzifanyia kazi kero zenu zote ambazo mmezitaja "alisema Loata 

Katika kikao hicho mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha alifuatana na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Musa Dadi Matoroka, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa anayewakilisha Mkoa wa Arusha Comrade Daniel Awaki, Robert Kaseko Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Olemoko Moloimet Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha, Yasmin Bachu - Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi ( UWT) Mkoa wa Arusha, Neema Mollel ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Arusha Ally Baro.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Comrade Loata Sanare akiongea na Wazee wakiwakilisha Makundi mbalimbali ya Wafugaji, Wanawake, Watumishi walioachishwa Kazi Katika Hifadhi ya Ngorongoro

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...