Na Woinde Shizza michuzi blog, Arusha
Chama cha waganga na wakunga wa dawa za tiba za asili jijini Arusha CHAWATIATA leo kimetoa tamko rasmi la kusisitiza kupewa leseni zao ambazo walizilipia kwa mda mrefu bila kuzipata na hivyo kupelekea kushindwa kufanya tiba kwa jamii kutokana na kutokuwa na leseni hizo
Akizungumza wakati wa mkutano uliowakutranisha waganga wa tiba za asili jijini Arusha katibu wa chama hicho Omar Mpera amesema kuwa kutopata leseni za kufanya tiba kumekwamisha shushuli zao na hivyo kurudi nyuma kimaendeleo
Aidha amesema kuwa wamezilipia miaka mingi iliyopita mara baada ya serikali kutoa tamko la kuwataka wawe na leseni hizo lakini hawajaona mrejesho wowote hivyo kukwama kufanya huduma ya tiba
Nao baadhi wa waganga wa tiba za asili jijini Arusha wamesema kuwa serikali imekuwa ikiwasahau hasa katika kukamilisha usajili wao na kupata leseni ambapo kwa sasa wamekata tamaa ya kufanya kazi zao kwa uweledi kwa kuhofia kuchukuliwa hatua kutokana na kutokuwa na leseni hizo
Hata hivyo wameahidi kuhuduia jamii kwa uwaminifu na kutumia miti shamba ambayo haina madhara kwa afya ya binadamu ili kuweza kunusuru maisha ya wananchi.
Badhi ya wanachama wa chama cha waganga na wakunga wa dawa za tiba asili mkoa wa Arusha
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...