Na Khadija seif, Michuzi tv
KUFIKIA uchumi wa viwanda kati pamoja na viwanda 2025 vyuo vikuu havina budi, lazima kuzalisha na kutengeneza wataalam wengi wasomi kutokea hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Makamu Mkuu wa chuo kikuu huria nchini Pro. Elifas Bisanda amesema kwa sasa wanafunzi wajikite kwenye masomo ambayo yataleta manufaa kwa mustakabali wa nchi kwa ujumla hasa masomo ya sayansi.
Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa chuo hicho kitatoa programu ya msingi ili kumuwezesha mwanafunzi kuwa na sifa za kuendelea na elimu ya juu.
"Kumekuwepo kwa changamoto tulizokumbana kutokana na Tume ya vyuo vikuu kufunga programu hiyo kwa muda wa miaka miwili kutokuwepo kwa program hiyo ya msingi (FOUNDATION COURSE) kwa wanafunzi ambao kimsingi walikosa sifa za kuendelea kwa masomo na kulazimika kurudi mtaani na kukatisha ndoto zao,"
Aidha, Bisanda amefafanua sifa za wanafunzi ambao wanaotakiwa kufanya udahili ni kwa wale ambao watakua wamefanya vizuri katika ngazi ya Astashada pamoja na wanafunzi waliohitimu kidato cha sita na kufaulu marks wanazohitaji ambazo ni nne zinazohesabiwa kwenye masomo mawili.
" Ni programu inayowaongezea maarifa wanafunzi ili kufikia kiwango Cha kujiunga na elimu ya juu, na sio programu rahisi Kama watu wanavyoitafsiri kwani wengi wao wamekua wakirudia mara kwa mara ili kupata sifa stahiki,"
Pia amebainisha kuwa programu hiyo ina masomo 14 ambapo masomo ambayo mawanafunzi inamlazimu kuyasoma masomo ya mazingira,tehama na Mawasiliano ili kumuandaa kulingana na ufaulu wake.
" Chuo chetu kinamuwezesha mwanafunzi kusoma mwenyewe kwa Mfumo wa tehama na kwa kutumia vitabu ambavyo vimechapishwa kwa moduli na kuendelea kusoma au kompyuta mpakato na simu janja wanaweza kupata mada zote ,"
Pia ametoa wito kwa wanafunzi wanaotaka kufanya udahili chuoni hapo kutokata tamaa kutokana na kukosa sifa na waanze na programu hiyo ya msingi na kumuwezesha kuendelea na elimu ya juu.
Makamu Mkuu wa chuo kikuu huria nchini Pro.Elias Bisanda akitolea ufafanuzi changamoto walizokua wakikumbana nazo wanafunzi walioachishwa masomo kutokana na kufutwa kwa programu ya msingi (FOUNDATION COURSE) na tume ya vyuo vikuu nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...