Anaandika Abdullatif Yunus wa MichuziTV - Kagera.
Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, ameongoza maafisa, askari wa Kikosi Na. 21 KJ, wananchi katika maadhimisho ya miaka 40 ya mashujaa Wa Vita ya Kagera, ambayo yamefanyika katika shamba la mashujaa Kaboya, Julai 25, 2019.
Katika Salaam zake Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewashukuru askari kwa kufanya kazi za kijamii ikiwa ni pamoja na kujitolea damu, huku akiwakumbusha askari hao juu ya majukumu yao ya ulinzi wa amani na mipaka ya Nchi yetu. Sambamba na hilo amewataka askari pamoja na majirani kuliona eneo la Kaboya na umuhimu wake kwa kulitunza na kulifanya la kihistoria akilifananisha na Eneo la Hijja kiimani, na kuahidi kuweka Nyumba ya kumbukumbu na historia ya Kikosi Na. 21KJ katika ushiriki wa Vita ya Kagera.
Vita ya Kagera ilianza mwaka 1978 Oktoba wakati ambapo Rais wa Uganda wakati huo Idd Amin Dada alipovamia ardhi ya Tanzania Mkoani Kagera eneo la Mtukula, eneo lenye Kilomita 1852, baada ya kuharibu Mali za wananchi, kuua wananchi, kuvunja daraja la Kyaka na kisha kubomoa Kanisa, na hapo ndipo Amir Jeshi wa Tanzania wakati huo Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na majeshi ya Tanzania yakiongozwa na Marehemu Jenerali Twalipo mnamo Novemba 1978 waliamua kutangaza vita ya Kagera iliyokusudia kumuondoa Idd Amin.
Katika Vita hiyo iliyomalizika Julai 1979 ilisababisha vifo vya askari wapatao 619, huku askari waislam wakiwa 258 na wakristo wakiwa 461. Mpaka sasa Mkoa wa Kagera umejiimarisha na kuendelea kuimalika kiulinzi ikiwa ni pamoja na ulinzi wa mipaka ya Nchi, na usalam wa Raia na Mali zao chini ya Vikosi vya ulinzi na Usalama.
Pichani Mnara wa mashujaa uliopo katika shamba la mashujaa Kaboya, walipozikwa askari waliofariki katika vita ya Kagera mnamo mwaka 1978-79.
Pichani Brigedia Jenerali Marco Gaguti Mkuu wa Mkoa Kagera akipata Maelezo kuhusu masalia ya zana za kivita zilizotumika kumuondoa Nduli IDD Amin na majeshi yake, wakati alipofika Katika shamba la mashujaa Kaboya Julai 25, 2019.
Pichani Brigedia Jenerali Gaguti akitoa heshima katika kaburi la Askari wa kwanza Kupoteza maisha katika Vita ya Kagera, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya Vita ya Kagera.
Pichani Brigedia Jenerali Marco Gaguti Mkuu wa Mkoa wa Kagera, akiweka Ngao na Mkuki Katika mnara wa mashujaa waliokufa katika vita ya Kagera, wakati wa maadhimisho ya Miaka 40 ya Vita ya Kagera.
Pichani ni Luteni Kanali Sadala Twalibu Kapungu Kamanda wa Kikosi 21 KJ, akiweka shada la maua katika mnara wa mashujaa waliokufa katika vita ya Kagera, wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya kumbukumbu ya Vita hiyo.
Pichani ni Askari wa Gwaride kutoka kikosi cha 21 KJ wakiwa katika gwaride la heshima katika shamba la mashujaa Kaboya, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 40 Vita ya Kagera.
Pichani Brigedia Jenerali Marco Gaguti Akipokea gwaride la heshima kutoka kwa kikosi cha 21 KJ, kabla ya ukaguzi wa gwaride hilo na kisha kutembelea makaburi ya mashujaa Wa vita ya Kagera.
Pichani Ni Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti pamoja na Kamanda wa Kikosi Na. 21 KJ Luteni Kanali Sadala Kapungu, wakiingia katika shamba la mashujaa Kaboya, walipolala askari waliopoteza maisha wakati wa Vita ya Kagera.
Sehemu ya Baadhi ya Askari, Wananchi, majirani na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kaboya, wakiendelea kumsikiliza Mgeni Rasmi wakati wa maadhimisho ya Miaka 40 ya kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita ya Kagera.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...